Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limesaini mikataba ya ubia na wabia kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 21 ambayo ina thamani ya zaidi bilioni 271 ikilinganishwa na thamani ya sasa ya majengo hayo ambayo ni bilioni 59.
Akizungumza katika hafla hiyo ya utiaji saini, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa amewapongeza wote walioshiriki kubuni wazo la kuihusisha sera ya ubia ya mwaka 2022 ambayo leo watanzania wameshuhudia utiaji saini wa utekelezaji wa sera hiyo.
“Juhudi za shirika letu la nyumba za kuwa wakereketwa wa maendeleo katika sekta ya nyumba ndiyo imetufanya tujumuike hapa leo kushuhudia mabadiliko haya makubwa hakika hili ni jambo jema”.
Alisema serikali inafahamu kuwa mlishawaalika wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuomba uendelezaji wa maeneo ya shirika yaliyopo katikati ya miji yetu.
Aidha, serikali iliwaagiza mhakikishe mnakuwa makini katika kuwachuja wabia hawa ili hatimae tuwapate waendelezaji makini na wenye uwezo wa kukamilisha miradi kwa wakati.
“Ni imani yangu kuwa maelekezo hayo yamezingatiwa vyema na hivyo leo kutufanya kushuhudia kundi la kwanza la wabia wanaoanza kutekeleza miradi itakayoongeza ufanisi kwa shirika na nchi yetu” alisema Waziri Silaa
Aliongezea kuwa serikali ilielekeza kuwapo umakini wa kuchuja waombaji wa miradi ya ubia kutokana na changamoto zilizojitikeza huko nyuma wakati wa utekelezaji wa miradi ya ubia.
Waziri Silaa alisema, sera ya ubia ya kwanza ya shirika iliyopitisha mwaka 1993 na kufanyiwa marekebisho kadhaa katika miaka ya 1998, 2006, na 2012 ilikuwa na changamoto mbalimbali kutokuwa na uwiano wa umiliki wa hisa za mradi, kutokuwa na kigezo cha thamani ya uwekezaji kwenye mradi ukilinganisha na thamani ya kiwanja cha shirika ili kuwa na mradi inayoendana na uwekezaji wa eneo husika.
Aidha, alisema sera hiyo haikuwa na vigezo vya kufanyiwa upekuzi yakinifu kwa makampuni yanayoomba miradi ya ubia ili kujiridhisha na uwezo wao wa kutekeleza miradi na iliruhusu baadhi ya wabia kutumia kati ya kiwanja cha shirika kama dhamana ya kupata mtaji wa kuwekeza kwenye mradi wa ubia.
Alisema, changamoto hizo zote zilizochangia miradi ya ubia kutokamilika kwa wakati sasa zimeondolewa katika sera hii mpya ya ubia iliyoboreshwa.
Hivyo, hatutarajia kuona hata mradi mmoja unasusua na tunatarajia miradi yote ikamilike kwa mujibu wa mikataba husika.
“Miradi inayotarajiwa kutekelezwa itaongeza idadi ya nyumba za kuishi pamoja na maeneo ya biashara na hivyo kuchangia kutatua changamoto ya makazi bora na maeneo bora ya biashara”
Pia huu ni utekelezaji wa maelekezo ya ilani ya uchaguzi wa chama cha mapinduzi CCM ya mwaka 2020 inayoelekeza kuongeza upatikanaji wa nyumba bora.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa NHC Hamad Abdallah alisema, sera ya ubia inalenga kujenga mazingira bora ya kibiashara, kuvutia wawekezaji na kuimarisha ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na jamii kwa ujumla.
Aidha, sera ya ubia ya NHC ilianza kutekelezwa kuanzia mwaka 1993, imekuwa ikifanyiwa maboresho mara kwa mara na maboresho ya mwisho yalifanyika mwaka 2022.
“maboresho hayo yalilenga kuondoa changamoto kadhaa amabazo zilikwamisha utekelezaji wa miradi hii ya ubia kwa ufanisi mkubwa”.
“kutokana na wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuyataka mashirika na taasisi mbalimbali za umma kushirikiana na sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo”
“Shirika la Nyumba la Taifa lilifanya maboresho makubwa ya sera yake ya ubia na maboresho hayo yalilenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa miradi ya ubia na kuongeza tija zaidi kwa shirika, wawekezaji na Taifa kwa ujumla” alisema Abdallah
Hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Hamad Abdallah alisema, maboresho yaliyofanyika yaligusa maeneo kadhaa ikiwemo kurekebisha uwiano wa umiliki wa hisa za miradi
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua