Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa Dkt. Sophia Kongela ametoa maelekezo kwa NHC akitaka kuhakikisha umuhimu wa kuimarisha utekelezaji wa miradi na ubora unaendelea kuzingatiwa kwa kila hatua.
Ameyasema hayo wakati ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya Shirika hilo iliyopo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kukagua maendeleo ya ujenzi ya miradi ya Kawe 711, Morocco Square, Samia Housing na eneo la NHC Urafiki ambayo inajumuisha ujenzi wa nyumba za makazi na biashara.
Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Sophia Kongela, amesema ni muhimu kwa Bodi yetu kufanya ziara kama hizi ili kujionea moja kwa moja maendeleo ya miradi yetu. Tunajivunia juhudi zinazofanywa na timu yetu ya ujenzi na tunahakikisha kwamba miradi yote inatekelezwa kwa viwango vya kimataifa.
Viongozi wa NHC waliokuwepo katika ziara hiyo waliweza kutoa maelezo ya kina kuhusu changamoto zinazojitokeza katika ujenzi na hatua ambazo zimechukuliwa ili kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati na kwa ubora unaotarajiwa.
Bodi inaendelea na ziara katika miradi ya Samia, Morocco Square na Eneo la NHC Urafiki kufuatilia utekelezaji wa maelekezo na miongozo yake.
Ziara hii ni sehemu ya juhudi za NHC katika kuhakikisha kuwa inatoa suluhisho la makazi bora kwa wananchi na kusimamia rasilimali za umma kwa ufanisi na uwazi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba