November 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Neema ya washukia wanawake wajasiriamali wilaya ya Magharibi ‘A’ Zanzibar.

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MKE wa makam wa Pili wa Rais Zanzibari Sharifa Omar Khalfan, leo amefunga mafunzo ya ujasiriamali ya Mwanamke Fanikisha yaliyokuwa yakiendesha kwa muda wa wiki moja na watoa mada tofauti katika ukumbi wa Abla apatiment.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, kwa ajili ya kuelimisha wanawake ili kuweza kuendesha biashara zao ikiwa ni moja kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Katika semina hiyo wajasiria mali wamefundishwa jinsi ya kulinda afya zao, Usafi wa mwili pamoja na mazingira kwa ujumla, kukuza mitaji yao, jinsi ya kuanzisha biashara.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo Mke wa Makamu wa Pili wa Raisi Sharifa Omar Khalfan, ameahidi kushirikiana na mkuu wa wilaya kuwafiki wajasiriamali waliopatiwa mafunzo hayo.

“Tunatakiwa kushikana mikono ili kufikia malengo katika biashara zetu nitaungana na Mkuu wa Wilaya Suzan Peter Kunambi, kuwafikia wote mlipata mafunzo haya ili kuboresha biashara zenu kulingana na mafunzo mliopatiwa,” anasema Sharifa Omar Khalifan.

Kwa upande wa muandaajia wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Magharibi ‘A’, Suzan Peter Kunambi, amewataka wajasiriamali hao kuunda vikundi kwa ajili ya kuwapatia mikopo ya kuendeleza biashara zao.

“Niwapongeze wote walioshiriki katika mafunzo haya hatua inayofwata muende mkaanzishe vikundi ambavyo tutakuja kuwa wezesha kwa ajili ya kuboresha biashara zenu.”

Mafunzo hayo yali hitimishwa na watoa mada mbunifu Martn Kadinda, Shande Yussuph na Mkuu wa Wilaya Suzan Peter Kunambi.