Na Nasra Bakari, TimesMajira Online, Dar es Salaam
RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameitaka serikali kutekeleza mradi mkubwa wa maji wa bwawa la kidunda ambao utawezesha kuwepo kwa uhakika wa maji katika kipindi chote cha mwaka katika jiji la Dar es Salaam na maeneo ya mkoa wa Pwani.
Ameyasema hayo jana tarehe 22 Machi 2022 alipokuwa akitoa hotuba yake katika kiulele cha maadhimisho ya wiki ya maji Mlimani City jijini Dar es Salaam Rais Samia alisema, tunakwenda kujenga bwawa la Kidunda ni la gharama na litachukua muda mrefu takribani miaka mitatu.
Rais huyo alisema, tutaanza kulijenga mwaka huu nadhani tutakwenda kumaliza mwaka 2025 litachukua muda mrefu lakini Dar es Salaam tutakuwa na uhakika wa kupata maji, lakini Maji ya bwawa hilo yatatumika kwa ajili ya matumizi ya binadamu, mifugo na kilimo.
“Aidha naipongeza Wizara ya Maji safi na Mazingira Dar es Salaam {DAWASA} kwa kazi nzuri inayofanya kwa mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Pwani, Chalinze, ambapo kwa sasa upatikanaji wa maji katika maeneo hayo upo katika viwango vya juu na kwa upande wa Dar es Salaam upatikanaji wa maji umefikia asilimia 96.
“Vilevile naielekeza Wizara ya Maji kufanya utafiti wa kuweza kutumia maji ya mto Rufiji ili uweze kusambaza maji Pwani, Rufiji hadi Dar es Salaam, ambapo pia ni mradi mkubwa na utatekelezwa na serikali ya awamu ya sita kwani maji ni uhai na hakuna mbadala wa maji,” alisema.
Alisema, Serikali anayoiongoza itaendelea kuiwezesha Wizara ya Maji ili iweze kwani kutekeleza majukumu yake ipasavyo, ambapo kwenye fedha za Uviko -19 serikali ilitoa Sh Bil.139 kwenda sekta ya maji, kwani maji ni uhai na ni kini paumbele cha serikali ya awamu ya sita.
Pia natoa wito kwa watanzania kutunza maxzingira hasda uoto wa asili ka kuepuka kukata au kuchoma miti ovyo au kufyeka misitu ovyo.
“Shughuli nyingine za kibinadamu karibu na vyanzo vya maji, hizi shughuli zinapelekea vyanzo kukata maji, “ alisisitiza Rais Samia.
Kwa upande wake Waziri wa Maji“Tuepuke Jumaa Aweso alisema, katika kipindi cha mwaka mmoja tangu Rais Samia ameingia madarakani Wizara ya Maji imakamilisha jumla ya miradi 463, pia inakwenda kutekeleza miradi 1176 ya maji na miradi 114 ya mjini.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa