Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Dar
WAZIRI wa Habari,Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Dk. Faustine Ndungulile amewataka wafanyabiashara ,wajasilimali pamoja na wananchi kujiunga na mfumo wa duka mtandaoni ili kuwawezesha kuuza na kununua bidhaa ndani na nje ya nchi.
Dkt.Ndungulile ametoa Rai hiyo jana katika maonesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa DITF yanayoendelea katika viwanja vya mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaama kwenye hafla ya utiaji saini ya makubaliano baina ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE) na Shirika la Posta Tanzania juu ya uendeshaji wa duka la mtandao.
Alisema duka mtandao ni fursa nzuri ya kufungua milango ya masoko ya kwa wajasiliamali wadogo wadogo na wakubwa kuuza bidhaa zao ndani na nje ya nchi.
“Kupitia duka mtandaoni wafanyabiashara watapata fursa ya kuuza bidhaa zao na mtu kupata fursa ya kuipokea popote pale anapokuwa japo hili ni nzuri na kusisitiza kuwa lengo la Serikali ni kuweka mabadiliko katika shirika la posta kuwa kitovu cha biashara”amesema.
Dkt Ndungulile amesema upo umuhimu kuanzisha sheria ya kusimamia taarifa binafsi .
Amesema Shirika la Posta imefungua zaidi ya vituo 350 na kununua magari 5 lengo kuhakikisha usafirishaji unafanyika kwa haraka na ufanisi.
Aidha ameitaka Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania kuwaamasisha wafanyabiashara kujiunga katika mtandao huu ili waweze kujitagaza na kuuza bidhaa zao.
Vilevile alisema kutokana na Teknolojia kukua kwa kasi ipo haja ya kutangaza maonesho haya kupitia mtandao ambapo mtu atapata fursa ya kuuza na kununua bidhaa popote alipo.
Katika hatua ameiomba Shirika la Posta Tanzania kuimarisha mifumo ili watu waweze kununua na kuuza bidhaa zao bila ya kupata chagamoto yoyote.
Kwa upande wake Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitlya Mkumbo matumizi mengi ya mitandao yamekuwa hayana maslahi katika kukuza uchumi.
Matumizi yetu ya mtandao zaidi yamejikita zaidi katika mambo ya kawaida yasiyokuwa ya kiuchumi badala ya kitumia katika shughuli za kiuchumi”alisema
Amesisitiz kuwa ni muhimu kutumia miundombinu ya kidijitali kuboresha uchumi ili kifikia malengo ya kimkakati.
Profesa Mkumbo amesema duka mtandao ni fursa nzuri ambayo itamuwezesha mfanyabiashara kufanya biashara bila ya kujenga duka.
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19