Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratibu Ummy Nderiananga amesifu maonesho ya wakulima (nanenane)ya mwaka 2024 huku akizitaka taasisi fedha kutoa elimu kwa wakulima na kuwawezesha kupata mikopo kwa masharti nafuu.
Nderiananga amesema hayo jijini hapa leo,Agosti 4,2024 alipotembelea Nzuguni katika maonesho ya wakulima maarufu kama nanenane ambapo pamoja na kutembelea mabanda mengine ili wakulima waendelee kuzalisha kwatija ni vyema wakapata mikopo nafuu itakayowawezesha kulima kilimo cha uhakika.
“Taasisi za mikopo zinatakiwa kutoa elimu kwa wakulima ili wasiogo kukopa kwani kuna mikopo nafuu,”amesema Nderiananga.
Pamoja na hayo Nderiananga ametembelea taasisi mbalimbali za umma na binafsi ambapo pia amepata fursa ya kukagua shughuli za kilimo zinazofanywa na taasisi zinazoshiriki maonesho hayo ya kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya nzuguni mkoani hapa.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano