November 15, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ndele Mwaselela: Dkt. Samia ameweka historia ya maisha yangu

Na Esther Macha, TimesMajira Online, Mbeya

MJUMBE wa halmashauri kuu CCM Taifa (MNEC)Ndele Mwaselela amesema kuwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amekuwa sehemu ya maisha yake na kuwa Mama mwema kwa kuweka historia ya maisha yake.

Ndele amesema kuwa kwake imekuwa bahati kwani yeye ni nani maana ni mtoto wa Mama Nitulie na Mlinzi ambaye amekuwa na dhamani kubwa mbele za watu.

Mwaselela amesema hayo Mei ,25 2024 wakati wa mahafali ya Seneti ya vyuo vikuu mkoa wa Mbeya yaliyofanyika ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya ambapo jumla wanachuo 1800 walitunukiwa vyeti.

Amesema kuwa Rais Dkt.Samia anasimamia wanyonge na amekuwa mtu wa kusimamia haki kuliko anavyofikiliwa na ni mtu makini anayejua thamani ya watu wa hali ya chini.

“Mwenyezi MUNGU hachagui anachotaka Moyo wake umwamini yeye na niliyesimama mbele yenu nimetoka kwenye familia maskini kabisa ,lakini MUNGU alisema maskini asiitwe milele na asife maskini hapa nilitaka niwape ujumbe muhimu kuwa wapo watoto wa maskini wakishikwa na kuwezeshwa wana uwezo mkubwa wa kuunganisha watanzania na kuweka mambo na kuhudumia watanzania wengi”amesema MNEC Ndele Mwaselela.

Aidha Mwaselela ameeleza kuwa ni wachache sana ambao hawaelewi lakini ukweli wa mambo ni kuwa wote wanaomwamini Mungu huinuliwa usiku na mchana na kwamba yeye ni sehemu ya maisha ya MUNGU kwa matendo ambayo amekuwa akifanya.

Hata hivyo Mwaselela amesema kwamba siku zote ukiwa mvivu na mchoyo na unajifungia baraka wenyewe hawataki kujifunza na wanaopata baraka ni wale wanaojitolea na kusema kuwa yeye alianza kujitolea kusaidia jamii mwaka ,2012 na mpaka sasa ana miaka 12 ,akiwa na shule moja ambapo mpaka Sasa ana shule tatu pamoja na miradi mbalimbali na bado anafanya kazi za chama na kusaidia watu .

Akielezea zaidi Mwaselela amesema Seneti ya mkoa wa Mbeya ni mfano kwa Tanzania nzima ambayo huwezi kuona popote zaidi ya Mbeya na kwamba ndo sababu yeye kama MNEC amewekeza kila nguvu yake ili kuhakikisha wanafunzi wa vyuo vikuu mkoa wa Mbeya hawapati tabu na kusema chama cha mapinduzi mkoa kitaendelea kuwapa ushirikiano na kazi ya mwanasiasa ni siasa sio kukaa ofisini.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu Taifa kupitia UVCCM mkoa wa Mbeya,Timida Mpoki Fyandomo amewataka wahitimu kwenda kuitumikia jamii katika kuimarisha na wakae wakijua kuwa Taifa linawategemea wasomi na kuwa mazuri waliyofanya wakiwa chama cha mapinduzi wakaendeleze katika jamii ili wananchi wafahamu kuwa Rais Dkt.Samia hajapoteza fedha kwa wasomi.

Baadhi ya wanavyuo wa Seneti ya mkoa wa Mbeya wakimsikiliza mgeni Rasmi katika mahali hayo Mnec wa mkoa wa Mbeya Ndele Mwaselela