January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ndele Mwaselela azindua mfuko wa udhamini wa masomo elimu juu

Na Esther Macha,Timesmajira Online,Mbeya

MAKAMUĀ  Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mt Augustino (SAUT) Prof .Coster RickyĀ  Mahalu amesema kutokana na changamoto za ukosefu wa mikopo ya elimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu wameweka mikakati ya kuanzisha mfuko kwa ajili ya kuendeleza wanafunzi wenye uhitaji wanaotoka familia zisizojiweza.

Prof.Mahalu amesema hayo leo wakati wa Uzinduzi wa mfuko wa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi sita wa Chuo hicho ulianzishwa na mdau wa elimu ,na Mkurugenzi wa Shule za ParadiseĀ  na Patrick Mission Ndele Mwaselela.

Aidha ProfĀ  Mahalu amesema kuwaĀ kwa upande wa ChuoĀ  sauti Jijini Mwanza asilimia 75 ya wanafunzi wa elimu ya juu ndo wamepata mkopo Serikali huku idadi kubwa wakiwa wamekosa na kukata tamaa na kuendelea na masomo.

Mkurugenzi wa Shule za Paradise na Patrick Mission ambaye ni mdau wa maendeleo Mkoa wa Mbeya ,Ndele Mwaselela amesema kuwa ameguswa kusaidia watoto hao kutokana na kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wa kike.

Amesema kuwa amefungua milango ili wadau wengine waweze kujitokeza kusaidia wanafunzi wenye uhitaji wapate elimu.

”Ndugu zangu kwaĀ  kipindi cha mwaka jana mpaka sasa Jumla ya 400Ā  wa elimu ya juu nimewaweza kuwafadhiri wanafunzi katika vyuo vikuu mbali mbali hapa nchini na sasa nimeanza kwa Chuo kikuu Kishiriki cha KatolikiĀ  Mbeya (CUCOM ”amesema Mwaselela.Ā 

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa kanisa katoriki na Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec)Gervas Nyaisonga amesema viongozi wa vyuo vikuu vya kanisa wasisite kuwashirikisha wadau kwani lengo ni kupaza sauti za wenye uhitaji.

Amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya idadi kubwa ya wanafunzi wanapata fursa ya elimu ya ya juu na kukosa mikopo SerikaliniĀ  jambo ambalo linalowafaya kughaili kuendelea na masomo kwa mwaka husika.

Nyaisonga amesema kuwa kitendo cha uongozi wa Chuo kutoa taarifa za kuwepo kwa changamoto hiyo Serikali na kumshirikisha mdau limekuwa chachu ya kusaidia wanafunzi sita kupata udhamini na kwamba wasisite kuendelea kupaza sauti kwa wadau kwani sio dhambi.

Mwanafunzi aliyepata udhamini wa masomo ,Grady Sanga ,amesema wamekuwa wakikataĀ  Ā tamaa kutokana na kukosa mikopo ya elimu ya juu na kwamba fursa hiyo waliyoipata itakuwa chachu kwao kusoma kwa bidii.