January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Ndege yapata ajali Mikumi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Ndege ya kampuni ya Unity Air 5H-MJH aina ya EMBRAER 120, iliyokuwa na watalii 30, marubani wawili na mhudumu mmoja imepata ajali asubuhi ya hii leo Novemba 28, 2023, iliyotokana na tatizo la kiufundi wakati ikitua katika kiwanja cha ndege cha Kikoboga kilichopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TANAPA imesema kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitokea Zanzibar, ambapo kutokana na juhudi zilizofanywa na marubani wa ndege hiyo pamoja na maafisa wa kiwanja hicho walihakikisha hakuna madhara yanayotokea ambapo watu wote waliokuwamo kwenye ndege hiyo walitoka salama na kuendelea na shughuli zao za utalii