*Ni mwendelezo wa utekeleza ahadi zake za kutatua kero za wananchi, sasa idadi ya ndege za ATCL zazidi kuongezeka
Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
NDEGE nyingine mpya ambayo imenunuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, inatarajiwa kuwasili nchini leo, ambapo itapokelewa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dtk. Philip Mpango.
Ndege hiyo aina ya Boeing 737 MAX 9 itawasili nchini leo ikitokea katika Mji wa Seatile, nchini Marekani ilikonunuliwa.
Kununuliwa kwa ndege hiyo kunalifanya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kupiga hatua baada ya mageuzi yaliofanywa na Serikali kwa kununua ndege hizo, ambapo mpaka sasa imeweza kuleta ndege 13.
Ndege hiyo aina Boeing 737 MAX 9 itafanya ATCL kuwa na ndege 14 kati ya 20 zinazohitajika. Hiyo itakuwa ni ndege ya pili zilizonunuliwa na Serikali kuwasili nchini mwaka huu, ambapo Juni, mwaka huu Rais Samia alipokea ndege ya mizigo mali ya ATCL aina ya Boeing 767-300F.
Akizungumza wakati wakati wa mapokenzi ya ndege hiyo, Rais Samia amesema Serikali itafanyia kazi ombi la kununua ndege nyingine ya mizigo.Aliwataka Watanzania kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali ili waendelea kufanya kazi na kutatua kero za wananchi.
Rais Samia alitoa kauli hiyo kufuatia ombi lililotolewa na Mkurugenzi wa ATCL, mhandisi Ladslaus Matindi, ambapo aliomba Serikali kuongeza ndege ya mizigo kutokana na kampuni hiyo kusaini mikataba na mashirika makubwa ili kufanya usafirishaji wa mizigo.
Ndege ya boeng 767 -300 F ina uwezo wa kubeba tani 54 za mizigo na hivyo kuja kwake kulisaidia kutatua changamoto ya uhaba wa ndege ya mizigo kutokana na Tanzania kuzalisha zaidi ya tani 24 za mizigo inayo paswa kwenda nje
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi