Na Mwandishi wetu,TimesmajiraOnline,Dar
NDEGE mpya ya abiria aina ya Boeing B737-9 Max ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambayo inatarajiwa kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam (JNIA) ni alama ya ushindi kwa Taifa
Akizungumza jana na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kuwasili kwa ndege hiyo ni muendelezo wa Serikali katika jitihada za kuboresha sekta ya uchukuzi ili kukuza uchumi wa nchi.
“Ujio wa ndege hii ni alama ya ushindi kwa Taifa, na fahari kubwa ,” amesema Chalamila.
Chalamila amesema aina hiyo ya ndege ni ya tatu kuwasili nchini tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani Machi 19,2021.
“Tulipokea Ndege ya kwanza ilikuwa ya abiria, ikaja ya mizigo na sasa hivi ni ndege ya tatu ya abiria lakini ni ya pili kwa aina ya Max,” ameesema Chalamila.
Amesema kuongezeka kwa ndege hiyo kunalifanya shirika hilo kufikisha jumla ya ndege 14; kati ya hizo moja ni ya mizigo na zinazobakia zinabeba abiria.
Kwa kujumuisha na uwekezaji huu sasa ATCL ina jumla ya ndege za abiria 12 na moja ya mizigo zinazohudumia vituo 24 kutoka vituo 19 vya mwaka 2021 na inatarajiwa vitaongezeka.
Kwa ujumla wake, ATCL imeongeza abiria kutoka 537,155 mwaka 2021 hadi 1,070,734; tani za mizigo 1,290 mwaka 2021 hadi 3,561; na miruko 10,550 mwaka 2021 hadi 17,198 mwaka
More Stories
Kapinga asema mafanikio katika sekta ya nishati yanatokana na jitihada za Rais Samia
Bumbuli kutekeleza miradi kwa kuangalia vipaumbele
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi