Mwandishi wetu, TimesMajira Online
SHIRIKA la Taifa la Maendeleo (NDC) limesema kwa mwaka wa fedha 2023/24 limejipanga kutimiza maono ya utekelezaji mradi wa liganga na mchuchuma ambao kwa miaka mingi ulikuwa ikikabiliwa na mikwamo licha ya kuwa na manufaa makubwa kwa uchumi wa nchi.
Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika hilo Dkt Nicolaus Shombe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji na vipaumbele vya NDC kwa mwaka 2023/24.
Amesema Kwa Sasa Shirika hilo limeweza kukamilisha majadiliano na mwekezaji na kusaini mkataba wa ubia huku majadiliano hayo yakitegemea kukamilika ndani ya mwaka wa fedha 2023/24 na hivyo kuruhusu hatua zinazofuata za uwekezaji.
“Kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe kupitia makampuni matano ambayo yamepatikana mwaka wa fedha 2022/23 ambapo jumla ya tani 315,000 za makaa ya mawe zinatarajiwa kuchimbwa katika mwaka wa fedha 2023/24 Kwa mradi wa mchuchuma na kulipa ada ya mwaka Kwa leseni ndogo za uchimbaji nje ya leseni kubwa katika mradi wa makaa ya mawe ya mchuchuma”amesema
Dkt Shombe alibainisha kuwa baada ya malipo hayo kukamilika Kampuni zitaruhusiwa kuendelea na uchimbaji wa makaa ya mawe .
Amesema utekelezaji wa mradi huo unatarajia kuchimba chuma tani milioni 2.9 kwa mwaka na kuzalisha bidhaa za chuma tani milioni moja kwa mwaka.
“Shirika limefikiwa kulipa fidia ya jumla shilingi bilioni 15.4 kwa wananchi wanaoishi mahali mradi unapotekelezwa wa miradi ya Mchuchuma shilingi bilioni 5 na Liganga shilingi bilioni 10 ambazo zimetolewa na serikali hadi kufikia Juni 30, mwaka huu na jumla ya wanufaika 1048 wamelipwa kati ya 1142,”amesema.
Aidha aliongeza kuwa licha ya kufanikisha kulipa fidia Shirika limefanikiwa kupata leseni Kwa ajili ya wachimbaji wadogo wa makaa ya mawe nje ya leseni kubwa ya mchuchuma.
“Upatikanaji wa leseni hizo unaliruhusu Shirika kuanza uchimbaji wa makaa ya mawe ambapo Kampuni tano za wazawa zinatarajia kuanza uchimbaji katika eneo la mchuchuma ndani ya mwaka 2023/24″amesema
Katika hatua nyingine Mkurugenzi huyo Mwendeshaji Dkt Shombe amesema katika kuunga jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kutokomeza ugonjwa wa Malaria NDC kupitia Kampuni yake tanzu y Tanzania Biolavides Product Limited (TBPL) inaendelea na uzalishaji na uuzaji wa viuadudu.
Amesema jumla ya Lita 68,494 za dawa za viuadudu zimezalishwa ambapo Lita 47,731.89 za viuadudu ziliuzwa ndani na nje ya nchi na kuingiza mapato ya jumla ya shilingi 1,696,619,665.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano