January 7, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nchimbi Katibu Mkuu Mpya CCM.

Na Penina Malundo.

KAMATI kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM,imemteua Emmanuel Nchimbi kuwa Katibu Mkuu Mpya wa CCM ambaye ameshika nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM,Daniel Chongolo aliyejiuzuru nafasi hiyo Novemba Mwaka jana.

NEC imemteua Emmanuel Nchimbi leo mjini Unguja , Zanzibar wakati wa kikao chake cha kawaida katika kujadili mambo mbalimbali ya chama chao.

Emmanuel Nchimbi sio jina geni katika masikio ya watanzania hususani katika nyanja ya siasa kwani tayari ameshika nafasi mbalimbali katika Serikali zilizopita.