Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online. Tanga
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amesema, hakutakuwa na Mabadiliko ya kweli katika kukuza uchumi wa nchi, endapo Sekta Binafsi hazitapewa kipaumbele katika uwekezaji nchini.
Dkt. Nchimbi ameyasema hayo leo Juni 8, 2024, Jijini Tanga wakati akizindua Kiwanda cha kuzalisha nyaya za umeme na kupeleka umeme Vijijini cha Tanga Cable kilichopo mkoani Tanga.
Nchimbi amesema, Serikali chini ya Chama cha Mapinduzi (CCM), itaendelea kusimamia sera yake ya kuhakikisha uwekezaji unafanyika nchini, ili kuweza kukuza uchumi wa Nchi, kwani ndiyo Ilani ya CCM inavyosema katika upande ufufuaji wa viwanda vilivyokufa na kuanzisha vipya.
“Napongeza za uongozi wa Tanga Cable kwa hatua hii nzuri mliyo chukua ya kuhakikisha mnawekeza nchini kwani kufanya hivyo kunaongeza kupanda kwa uchumi nchini na hakutakuwa na Mabadiliko ya kweli katika kukuza uchumi wa nchi, endapo Sekta Binafsi hazitapewa kipaumbele katika uwekezaji nchini”, Amesema Dkt. Nchimbi.
Aidha, ametoa wito kwa Taasisi za Kiserikali, Sekta Binafsi na Wananchi kwa ujumla, kujenga utamaduni wa kutumia bidhaa za ndani baada ya kujiridhisha ubora wake, ili viwanda viendelee kujua na uchumi upande.
Ameongeza kuwa, uwepo wa viwanda vingi nchini, kutasaidia kuongezeka kwa ajira, kupunguza usumbufu na gharama za uagizaji wa bidhaa nje ya nchi.
Awali Akizungumza katika uzinduzi wa Kiwanda hicho, Mkurugenzi wa Tanga Cable, Murtaza Dossaji, amesema, Kiwanda hicho kipo kwa takribani zaidi ya miaka 60 nchi Tanzaniana, huku uwekezaji wake ukiwa ni zaidi ya bilioni 1.
Amesema, Tanga Cable ni miongoni mwa viwanda bora nchini, ambapo pia kinaenda kutoa ajira kwa zaidi ya watu 50, huku akidai kuwa nia ya Kiwanda hicho ni kuboresha Sekta katika Sekta ya Nishati ya Umeme nchini.
“Kiwanda hiki ni zao la Tanzania na ni cha miaka mingi na lengo letu no kukuza Sekta ya Nishati ya Umeme nchini kwa upatikanaji wa nyaya kwa bei nafuu na tunatarajia kuajiri zaidi ya wafanyakazi 50”, Amesema Dossaji.
Dossaj pia, ameishukuru Serikali chinj ya Rais Dkt. Samia, Uongozi wa Rais Samia kuwawezesha wazawa na wadau wa maendeleo kwa kuwapatia mazingira rafiki kwenye uwekezaji sekta ya viwanda.
Pia, amewaomba Wakandarasi kuweza kuunga mkono juhudi za Tanga Cable kwa kununua nyaya hizo, ambazo amedai kuwa bora na zenge bei nafuu ili kukiwezesha Kiwanda kuongeza Pato katika Jiji la Tanga.
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu