December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NCCR Mageuzi wamtuhumu James Mbatia

Na Bakari Lulela, TimesMajira Online

CHAMA cha NCCR Mageuzi kinamtuhumu aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia aliposimamishwa uongozi na mkutano mkuu ulifanyika Septemba 24 mwaka 2022 jijini Dodoma kwa utovu wa nidhamu na uporaji wa Mali za chama.

Akizungumza jijini Dar es salaam, katibu mkuu wa chama hicho Faustian Sungura amesema mkutano mkuu uliuagiza uongozi wa chama kumchukulia hatua za kisheria James Mbatia ikiwa pamoja na kuhakikisha Mali alizopora zinarejeshwa kwenye chama.

“Baada ya chama kukusanya vielelezo na ushahidi kilianza kumchukulia hatua James Mbatia kwa kwenda wilaya ya kipolisi ya Mbeleni machine 28hadi 29 mwaka huu kwa ajili ya kufungua jalada la kujimilikisha nyumba mbili za chama na kunipatia sh 67000,000 kwa nji za udanganyifu,”amesema Sungura 

Aidha chama hakikubaliani na hujuma hizo utaratibu wa kukishirikisha chombo cha serikali jeshi la polisi kuweza kifuata mkondo wa Sheria ufuatwe pia waliruhusu kutumika njian nyingine ya kurejesha nyumba 2 za chama.

Hata hivyo chama cha NCCR Mageuzi kinawataka wavamizi wote wanaoshi au kufanya biashara kwenye nyumba hizo wawe wameondoka kabla ya julai 30 ,mwaka huu Ili kupisha ukarabati mkubwa unaotarajiwa kuanza agosti Moshi ambapo watapeleka notisi ya kuwataka wahame mara moja.

Kiongozi huyo aliendelea kusema kuwa pamoja na ofisi ya RCO wa kinondoni kumlinda James Mbatia Ili asifikishwe kwenye chombo cha kutoa haki,(mahakamani) chama bado kina Imani na ofisi ya DPP wa mkoa wa kinondoni.

Hivyo tunakwenda kufungua jalada dhidi ya James Mbatia, kwa kupora na kuuza shamba la chama lenye ukubwa wa hekari 56 katika Kijiji cha kiromo wilayani Bagamoyo.ambapo CAG amethibitisha kuwa halikuwa Mali ya James Mbatia.

Katibu mkuu wa chama cha NCCR Mageuzi Faustian Sungura akielezea hujuma zilizo fanywa na aliyekuwa mwenyekiti James Mbatia za kupora na udanganyifu dhidi yake