Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimesema kitashiriki mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) unaotarajiwa kufanyika jijini Dodoma kuanzia Machi 30 hadi 31 mwaka huu.
Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam jana Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma Taifa wa chama NCCR Mageuzi , Edward Simbeye amesema Chama hicho ni miongoni mwa Vyama vitano vitakavyoshiriki katika mkutano huo baada ya Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi juzi kuridhia kufuatia matakwa yao waliyotaka yafanyiwe kazi ili waweze kushiriki kutekelezwa.
Amesema miongoni mwa matakwa ambayo walitaka yafanyiwe kazi ni pamoja na kutaka Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe aachiwe huru bila masharti.
Mengine ni walitaka kikao hicho cha TCD kisiitwe kongamano na badala yake uitwe ni mkutano ili vyama vya Siasa viutumie kujadiliana mambo mbalimbali na kupata muafaka.
Simbeye amesema lingine walitaka kabla ya kufanyika mkutano huo lazima viongozi wa vyama wanachama wa TCD wakutane na Rais Samia kabla ya kufanyika mkutano huo jambo ambali limekubaliwa kwani watakutana na Rais Machi 18 mwaka huu.
“ Kamati Kuu imesema hoja zetu zote zimezingatiwa, kwahiyo tutashiriki mkutano huo kama mwanachama halali wa TCD,” amesema Simbeye.
Vilevile amesema kuwa bado kuna uhitaji wa kuwepo kwa muafaka wa kitaifa.
More Stories
Rais Dkt.Samia asajili timu ndani na nje ya Nchi kukabili Marburg
RUWASA Katavi yasaini mkataba ujenzi bwawa la Nsekwa
Wapanda miti 500,kumbukizi ya kuzaliwa Dkt.Samia