May 17, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBAA, ZIAAT wasaini hati ya makubaliano ya kufanya kazi pamoja

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) na Taasisi ya Wahasibu, Wakaguzi na Washauri elekezi wa kodi Zanzibar (ZIAAT) wamesaini hati ya makubaliano ya miaka minne ya kufanya kazi pamoja kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo uandaaji na uendeshaji wa mafunzo endelevu katika nyanja za Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu.

Makubaliano hayo ya miaka minne ambayo yapo huru kuendelezwa na kuongezewa muda pindi makubaliano ya awali yatakapofikia ukomo, Hii ni hatua nzuri na kubwa kwa ukuaji na uendelevu wa Taaluma ya Uhasibu nchini.

Aidha, makubaliano hayo yatasaidia kurahisisha utendaji kazi wa Taasisi hizi mbili kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Ikumbukwe ya kwamba Sheria iliyoanzisha NBAA ilikuwa inaishia Tanzania Bara.

Pia kuanzishwa kwa ZIAAT upande wa Zanzibar pamoja na kusainiwa kwa makubaliano hayo, yatasaidia NBAA kufanya kazi Zanzibar kwa kushirikiana na ZIAAT, pia ZIAAT kufanya kazi Tanzania bara ikishirikiana na NBAA.

Hivyo, kwasasa Taasisi hizo zimekubaliana kushirikiana katika mambo mbalimbali ikiwemo uandaaji na uendeshaji wa mafunzo endelevu, Masuala ya uanachama, Masuala ya mitihani na Masuala ya ufundi.