November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBAA yawataka vijana kuchangamkia fursa za uhasibu,ukaguzi

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imewahimiza vijana wa kitanzania nchini kuchangamkia fursa za uhasibu na ukaguzi kutokana na kuwa na mchango mkubwa katika maendeleo endelevu ya Taasisi, makampuni ili kuleta tija kwenye ukuaji wa uchumi na ujenzi wa Taifa.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) CPA Prof. Sylvia Temu, Julai 6, 2024 Jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Julius Nyerere.

“Tunasimamia vigezo vya uandaji wa hesabu za kimataifa na kuhakikisha wanachama wetu wanazingatia maadili na vile vigezo ambavyo vinafanya tasnia ya uhasibu iwe na heshima na mchango unaotarajiwa na wananchi” amesema CPA Prof. Sylvia Temu

Prof. Sylvia Temu ameongezea kuwa ushiriki wao katika maonyesho hayo ni kutoa elimu na kusikiliza sana wadau ili kupata maoni ya mbalimbali na wanatoa mrejesho gani juu ya kazi zinazofanywa na NBAA ili kuboresha zaidi kazi zetu.

Hivyo, Prof. Temu amesema kila kitu kinachofanywa ni lazima kuzingatia viwango ambavyo vinavyosisitiza uendelevu wa huduma, uzalishaji na utunzaji wa mazingira.