Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online DSM
BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu Tanzania (NBAA) imetoa mafunzo kwa wanafunzi wa Baobab kwa lengo la kuwajengea uwezo juu ya uelewa wa masomo ya uhasibu ikiwa ni muendeleo wa Taasisi hiyo kutoa elimu kwa Vyuo pamoja na Shule za Sekondari ili kukuza taaluma ya Uhasibu Nchini.
Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo Mkurugenzi wa Huduma za Shirika CPA Kulwa Malendeja alitoa salamu kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), CPA Pius A. Maneno ambaye alitamani kuwepo kwenye mafunzo hayo lakini kutokana na majukumu mengine ameshindwa.
Pia amesema si kila aliyesomea uhasibu anaweza kuwa Mhasibu bali inabidi kufanya mitihani ya Bodi hiyo ili kupewa cheti cha kitaaluma ili uweze kutambulika kama Mhasibu na kuweza kufanya kazi nje na ndani ya nchi.
Aliongeza kuwa wanafunzi wa Kozi nyingine ambazo hazihusiani na masomo ya Uhasibu nao wana nafasi ya kufanya mitihani ya Bodi na wataanzia masomo ya ngazi ya kwanza (foundation level) tofauti na wale waliosomea masomo ya Uhasibu na pia waliomaliza kidato cha nne na sita na wanacheti wanaweza kufanya mitihani ya Bodi alisema Malendeja.
Akiishukuru NBAA, mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi amesema Bodi kwa mwaliko wa wanafunzi ili kuja kupata Elimu ya Uhasibu.
Aliongeza kuwa wanafunzi waliotembelea Bodi ni wanafunzi wa kidato cha tano wa wanaosoma masomo ya biashara katika shule hiyo ambao itawapa dira na mwelekeo mzuri sasa na hapo baadae.
Mkurugenzi wa Huduma za Shirika CPA Kulwa Malendeja akizungumza kwa kuwakaribisha pamoja na kufungua mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (​NBAA), CPA Pius A. Maneno kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea NBAA.
Afisa Utumishi kutoka NBAA, Gloria Kaaya akizungumza na wanafunzi wa Baobab wa kike na kiume kukazania masomo yao kwani wapo kwenye njia sahihi na kuwasisitiza Wanawake kupambana ili kufikia idadi sawa na wanaume katika taaluma ya Uhasibu na ikiwezekana kuwazidi kwa asilimia 70 kwa 30.
Afisa Uhusiano na Mawasiliano wa NBAA Magreth Kageya akizungumza kuhusu historia ya Bodi na kazi zinazofanywa na Bodi hiyo pamoja na faida za kuwa na CPA wakati wa mafunzo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara kutoka Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea ofisi zao kwa ajili ya kupata mafunzo.
Afisa Elimu Mwandamizi kutoka Kurugenzi ya Elimu na Mafunzo NBAA Heri Mnzava akitoa mafunzo kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab kuhusu hatua mbalimbali za mitihani ya Bodi hadi kufikia CPA yaani kuanzia ile ya ngazi ya utunzaji vitabu vya fedha hadi ngazi ya taaluma.
Mhasibu kutoka NBAA, CPA Yusuph Lema akiwasilisha mada kuhusu uandaaji wa Taarifa za hesabu za fedha kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo.
Mkaguzi wa ndani wa NBAA CPA George Lazaro akitoa elimu kuhusu ukaguzi na kazi za wakaguzi kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab waliotembelea na kupata mafunzo katika ofisi za Bodi ya NBA.
Baadhi ya walimu pamoja na wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab wakifuatilia mada zilizokuwa zinatolewa na maafisa mbalimbali kutoka NBAA.
Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Baobab Stephen Gervas Mahundi akitoa neno la shukrani kwa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu Tanzania (NBAA) mara baada ya wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara kutoka Shule ya Sekondari ya Baobab kumaliza ziara yao walipotembelea ofisi za Bodi ya NBAA zilizopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya watumishi wa NBAA wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walimu pamoja na wanafunzi wa Kidato cha Tano wanaosoma masomo ya Biashara katika Shule ya Sekondari ya Baobab.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano