December 27, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NBAA yatangaza matokeo ya mwezi Novemba 2023

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

BODI ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imeidhinisha matokeo ya mitihani ya 98 iliyofanyika mwezi novemba ya Bodi ambapo takwimu zinaonesha watahiniwa 6711 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi ufaulu ni asilimia 66.6

Ameyasema hayo Mkurugenzi Mtendaji wa NBAA CPA Pius Maneno leo Desemba 21, 2023 jijini Dar es Salaam wakati akiidhinisha matokeo hayo amesema Ufaulu umepungua kutoka asilimia 67 mpaka 66.6 ambapo watahaniwa 527 hawakuweza kufanya mitihani kwa sababu mbalimbali, hivyo idadi ya watahaniwa 6711 sawa na asilimia 92.7 walifanya mitihani ambapo wanawake walikuwa 3636 sawa na asilimia 50.2 na wanaume 3602 sawa na asilimia 48.8

CPA Maneno Amesema bodi inaendelea kuboresha mitaala ya kufundishia ili kuongeza idadi ya wahasibu hapa nchini na waweze kuchangia katika maendeleo hasa kuhakikisha hesabu tunazozitoa zinakuwa ni sahihi na zinaaminika.

Hivyo, CPA Maneno amesema wataendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu kuhakikisha maadili yanazingatiwa ili vijana waandaliwe tangu wakiwa vyuoni.