Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM
Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA) imeidhinisha matokeo ya mitihani ya 97 ya Bodi kwa Watahiniwa waliofanya mitihani hiyo iliyofanyika mwezi Mei 2023 katika ngazi mbalimbali za masomo ya Bodi.
Ufaulu umeendelea kuongezeka tofauti na mwaka uliyopita kwa watahaniwa waliosajiliwa 6,837 na watahaniwa 505 hawakuweza kufanya mitihani kwa sababu mbalimbali, hivyo idadi ya watahaniwa 6,332 sawa na asilimia 92.6 walifanya mitihani wanawake walikuwa 3,112 sawa na asilimia 49.1 na wanaume 3,220 sawa na asilimia 50.9
Ameyasema hayo Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya NBAA CPA Prof. Sylvia Temu kuwa kati ya watahiniwa 4,205 sawa na asilimia 66.4 wamefaulu mitihani yao na watahaniwa 2,127 sawa na asilimia 33.6 hawakufaulu mitihani hiyo.
“Bodi inawapongeza wale wote waliofaulu mitihani yao na kuwataka wale ambao hakufaulu kutokata tamaa bado waongeze bidii na sisi kama bodi tutawapa msaada mkubwa kuhakikisha wanapata rasilimali mbalimbali za kujisomea na kujifunzia kama maktaba” amesema Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Temu
Ameongezea kuwa huu ni mchakato na tunaamini watafaulu ili tuongeze idadi ya wahasibu hapa nchini na waweze kuchangia katika maendeleo hasa kuhakikisha hesabu tunazozitoa zinakuwa ni sahihi na zinaaminika.
Aidha, CPA Prof. Temu amesema wameendelea kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu kuhakikisha tunazingatia suala la maadili katika mafunzo ili vijana waandaliwe vizuri tangu wakiwa vyuoni tunasisitiza sana kwa sababu hiyo ni sehemu kubwa ya uhasibu na ukaguzi wa hesabu.
Hivyo, bodi inapenda kuwafahamiaha watahaniwa pamoja na umma kwa ujumla kuwa bodi ipo katika zoezi la kuboresha mitaala ya masomo ambayo itaanza kutumika kuanzia muhula wa mitihani ya novemba 2024.
More Stories
Mwanasiasa mkongwe afariki Dunia
Rais Samia Kuzindua Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM