Na Penina Malundo, timesmajira
WAZIRI wa habari Mawasiliano na Teknolojia ya habari Nape Moses Nnauye ameupongeza uongozi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL ) kwa kazi kubwa na nzuri walioifanya katika suala zima la mawasiliano nchini.
Pia amewataka wafanyakazi pamoja na viongozi wa Shirika hilo kuendelea kuboresha huduma za mawasiliano na kuwaunganisha wateja wote kwa wakati.
Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam amesema kukua kwa teknolojia ndio lengo la nchi hivyo TTCL inapaswa kuendelea kubaki kileleni kama walivyofanikiwa kufika Internet katika kileleni Cha mlima Kilimanjaro.
Nape amesema shirika hilo linazidi kupiga hatua siku hadi siku katika kuhakikisha Mawasiliano nchini Tanzania yanakuwa mazuri na yanawafikia watanzania kwa uhakika.
Awali akitoa maelezo ya utangulizi , Mkurugenzi wa TTCL Injinia Pitter Ulanga amesema katika maonesho ya Mwaka huu wamekuja ni vitu mbalimbali kuwaoneshea Wananchi wanaofika katika Banda lao ikiwemo simu ya zamani katika kwa lengo la kuonesha asili ya Mawasiliano yalipoanzia.
Amesema kuwa mawasiliano yalikuwepo kabla ya miaka 100 na kuhakikisha serikali kupitia Shirika la mawasiliano litaendeleza juhudi za kuhakikisha wananchi wanapata mawasiliano kwa zaidi ya miaka 100.
Amesema kuwa TTCL inafungua milango ya kidigital Tanzania na kwa kuhakikisha Hilo tayari katika shirika mteja anapata huduma ya vedio conference pamoja na hologram akiwa sehemu yeyote Ile.
Aidha Mkurugenzi wa TTCL ameshukuru serikali kwa kuwarudishia mkongo wa Taifa na kuahidi watahakikisha wanaendelea kutoa huduma za wasialiano kwa wananchi wote watanzania na nje ya Tanzania.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi