Na Esther Macha,TimesMajira,Online,Mbeya
NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi,Maryprisca Mahundi ametoa wiki mbili kwa Meneja wa wakala wa maji vijijini (RUWASA),Mkoa wa Mbeya Mhandisi Hans Patrick,kuhakikisha miradi mitatu ya maji katika Kata ya Iwindi unakamilika na wananchi wa vijiji sita vya kata hiyo wanapata maji.
Naibu Waziri huyo amesema hayo jana akiwa Mkoani Mbeya katika ziara yake ya siku tatu ya kukagua miradi ya maji iliyopo katika Mkoa wa Mbeya na wilaya zake .
Hata hivyo Mhandisi Mahundi amesema kuwa anafahamu mradi huo unatakiwa kutoae maji kwa vijiji nane (8) lakini vijiji sita (6) angalau ndani ya wiki mbili maji yanatoka kwa vijiji sita.
Aidha Mhandisi Mahundi amevitaja vijiji hivyo kuwa ni Horonga,Itimu,Iwindi,Mwambalala,Izumbwe,Mwashiwalala na kusema kuwa vijiji hivyo vina uwezo wa kupata maji kwa wiki mbili.
“Mheshimiwa Rais Magufuli ana vijana ambao wapo tayari kuona wanatatua changamoto za wananchi ,huyu ni Mhandisi wa mkoa wa Mbeya ameweza kufanya vizuri mkoa wa Ruvuma na sasa tumeletewa Mbeya atusaidie tupeni Imani kwani waliokuwepo wameondolewa kutokana na uzembe huyu Mhandisi tumpe ushirikiano maji yatoke bombani Hawa akina mama inatosha kubeba maji vichwani”amesema Naibu waziri.
Akifafanua zaidi Mhandisi Mahundi amesema rais alishaleta zaidi ya sh.Bil.3 na kwamba sababu fedha zipo ila kulikuwa mzembe mmoja ambaye ameondolewa maji sasa yatatoka.
Kuhusu vijiji viwili vya Shongo na Igale vilivyopo mlimani Naibu Waziri amesema kuwa Rais Magufuli ametoa sh.Mil.26 na kifaa tayari kimeshanunuliwa cha kitaalam ili kiweze kufungwa na maji yaweze kupanda kwenye mlima.
Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya Vijijini,Oran Njenza amesema kwamba tatizo la maji kwa Iwindi na Igale ni sugu na kwamba Serikali ilitoa zaidi ya sh.Bil.3 lakini wananchi hawajawahi kufaidi maji licha ya mradi huo kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Iwindi ,Mfisile Nswila amesema kuwa maji ni tatizo kwani yanaweza kutoka yakachukua hata miezi mitatu bila maji kutoka pamoja na kuwa mradi kuwa wa mabilioni ya fedha lakini haijasaidia wana Iwindi .
More Stories
Mjumbe wa Baraza UWT ahimiza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â