Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
Naibu Waziri wa Tamisemi Festo Ndugange amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya kituo kipya cha Afya kata ya Vunta, wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa kituo hicho akiambatana na Mbunge wa Same Mashariki Anne kilango, Naibu Waziri Dkt. Dugange amesema serikali imetoa milioni mia tatu za awali kujenga kituo kipya cha Afya vunta ambacho kitajengwa na jengo la upasuaji na chumba cha kuifadhia Maiti.
Aidha, ameendelea kusema fedha hizo zimetolewa na Raisi Samiha Suluhu Hassani kuhakikisha wananchi wa kata ya vunta wanapata Huduma bora ya Afya, pia akiwa kwenye ziara hiyo amemshukuru Anne kilango kwa juhudi kubwa anazofanya kuwapambania wananchi wa jimbo lake akiwa bungeni.
Ameongezea nakusema amevutiwa na miradi mikubwa ya jimbo hilo ikiendelea vizuri ujenzi wa Madasa ya Shule ya Sekondary ya Mihamba na zahati kubwa na ya kisasa ambayo imegharimu milioni mia tano za ujenzi wake na ukikalibia kukamilika hivi karibu.
Hivyo, serikali itashirikiana na Tarura kuhakikisha barabara zote ambazo zinajegwa ili kuleta unafuu kwa wakazi wa vijiji vya Same Mashariki kakamilika kwa wakati.
Naibu waziri Festo amewaomba wananchi wa jimbo la Same Mashariki kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake
kwa upande wake Mbunge wa Same Anne kilango amesema anatoa shukran sana kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumpatia milion mia tatu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya vunta ambacho alikisemea akiwa bungeni zaidi ya mara tatu na leo utejelezajiwake unakwenda kukamilia.
Pia ameendelea kusema lengo lake ni kuona wananchi wake hawapati tabu kwenye mahitaji muhimu kama Afya, Elimu, Maji, na barabara ili waweze kupitisha mazao yao kwa wepesi zaidi na ataendelea kuwapatia wananchi wake miradi tofauti wajikwamue kiuchumi.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa