December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Waziri Mavunde afungua mkutano wa wazalishaji Tumbaku

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Peter Mavunde leo amefungua mkutano wa siku 2 wa nchi wazalishaji wa zao la Tumbaku kusini mwa jangwa la Sahara ambazo zinajulikana kama T5 .

Mkutano huo umefunguliwa leo katika Hotel ya Mount Meru Jijini Arusha ukihudhuriwa na wawakilishi kutoka nchi za Tanzania, Zimbabwe, Malawi, Zambia na Msumbiji ambao pia una dhamira ya kutengeneza sauti ya pamoja ya mkakati wa utekelezaji wa Mkataba wa Kimataifa wa Shirika la Afya Duniani( WHO ) juu ya udhibiti wa matumizi wa matumizi ya Tumbaku.