Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja (Mb) amekabidhi vifaa mbalimbali vya mazoezi ya viungo kwa watoto wenye ulemavu wanaoishi pembezoni mwa Pori la Akiba la Pande ikiwa ni sehemu ya tamasha la kuhamasisha utalii wa ndani.
Tamasha hilo limefanyika Novemba 19,2022 lilihusisha utalii wa michezo ya mbio za baiskeli na mbio za kukimbia kwa miguu katika Pori la Akiba la Pande jijini Dar es Salaam.
“Washiriki wote waliokimbia mbio za baiskeli kilomita 33, Mbio za kukimbia kwa miguu kilomita 21,10, na 5 kiingilio kilichotoka kimeweza kuchangia upatikanaji wa vifaa vya hawa watoto wenye ulemavu” Mhe. Masanja amesisitiza
Aidha,amewahamasisha watanzania wengine wenye uzalendo kuendelea kujitokeza kuchangia kundi hilo la watoto wenye ulemavu.
Amesema matamasha kama hayo yataendelea kufanyika katika maeneo mengine ya hifadhi ili kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii nchini na kufungua fursa za uwekezaji.
Naye kamanda wa kanda maalum ya uhifadhi ya Dar es Salaam (TAWA) Sylvester Mushi amesema kuwa wananchi mbalimbali walishiriki mbio hizo kwa lengo la kuchangia kiasa cha fedha ili kusaidia watoto wenye ulemavu ambao wapo kando kando la pori hilo, kwahiyo hii ni sehemu kubwa kwa wale waliokimbia katika kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Kwa upande wake Mwakilishi wa AFIC Tanzania anampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali watu wenye ulemavu kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali, pia ametoa rai kwa wananchi na makampuni mbalimbali kuwaunga mkono milango na ipo wazi ili kuweza kuwasaidia watoto wenye ulemevu.
Tamasha hilo lilihusisha washiriki kutoka maeneo mbalimbali nchini kutoka katika Taasisi za Serikali na Zisizo za Kiselikali.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto