November 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Waziri MaryPrisca apokea msaada wa majiko ya gesi

Na Esther Macha,TimesMajira Online,Mbeya

NAIBU Waziri wa Maji Mhandisi MaryPrisca Mahundi amepokea msaada wa majiko ya gesi ya Oryx 500 kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Tanzania ,Araman Benoit kwa ajili ya wanawake ili waweze kutunza mazingira katika maeneo yao.

Naibu Waziri wa Maji Mhandisi MaryPrisca Mahundi akipokea msaada wa majiko ya gesi 500 kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Oryx Tanzania ,Araman Benoit kwa ajili ya wanawake ili waweze kutunza mazingira

Amesema kuwa akiwa kama Naibu waziri wa maji anapenda kuona kuwa mazingira yanatunzwa na kupeana utamaduni wa kuona kuwa kila mwananchi anakuwa rafiki wa mazingira na wizara ya maji wanajitahidi kuwa rafiki wa kutunza mazingira.

Akipokea msaada huo jana mhandisi Mahundi amesema kuwa alipata wazo hilo kutukanana na kuwa.kumwakilishi wa wanawake wa mkoa wa Mbeya.

Aidha Mhandisi Mahundi amesema kuwa wanawake ndo watunzaji wa mazingira namba moja na wanawake ndo waandaji wa chakula katika familia na kwamba wanawake walio wengi wapo nje ya mji ambao asimilia kubwa wanatumia kuni pamoja na mkaa.

“Dhamira ya kuona hii kampeni ya kupunguza matumizi ya mkaa na kuni na kuwaingiza wanawake kwenye mwamko na kuona kuwa wanawake wanaweza kutumia gesi Kama nishati mbadala namshukuru sana mkurugenzi mkuu wa Oryx kwa kukubaliana na mawazo yangu mimi mwakilishi wa wanawake Mkoa wa mbeya”amesema Mhandisi Mahundi.

Akielezea zaidi Naibu waziri wa maji amesema kuwa wanaenda kuanza zoezi la kukabidhi majiko ya gesi 500 wanawake hao wanakwenda kuwapata kote za mkoa wa mbeya na majimbo yote na kuwa kila wila atagawa majiko ya gesi 50.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Tanzania ,Araman Benoit amesema kuwa baada ya kupokea maombi kutoka kwa Naibu waziri wa maji Mhandisi Mahundi wanaungana nae katika kampeni ya utunzaji mazingira na hivi sasa huduma yao gesi ya Oryx inapatikana mpaka vijijini.

Hata hivyo Benoit amesema kuwa wamewekeza sana maeneo yote katika kulinda mazingira ,pia kukuza uchumi wa Tanzania hususan wanawake wa Tanzania.

“Oryx pia wamewekeza kukuza ajira kwa vijana ,pia wabajivua jitihada za Naibu waziri katika kulinda mazingira hivyo tutahakikisha tunakuwa pamoja nae katika harakati alizoanzisha”amesema mkurugenzi mkuu Oryx.