January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Waziri Kapinga atoa maelekezo TANESCO

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Naibu waziri wa Nishati Judith Kapinga, amewaelekeza TANESCO kuweka mfumo ambao ni sahihi wa kukata na kurudisha umeme ili shughuli za uzalishaji ziweze kuendelea.

Maelekezo hayo ameyatoa jana Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ziara aliyoifanya katika kituo Cha kuzalisha umeme Tegeta chenye mitambo mitano inayozalisha Megawati 43 ambapo ni Megawati 8.3 kwa kila mtambo na kueleza kuwa Serikali itanaendelea kusimamia kuhakikisha huduma ya upatikanaji umeme inaendelea kuimarishwa kwa kusimamia matengenezo kama ambayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alielekeza lakini pia tunaendelea kufatilia uzalishaji kwa kiasi kikubwa.

“Hali ya uzalishaji katika kituo hiki Cha hapa Tegeta ni nzuri, mitambo minne inafanya kazi na Mtambo mmoja ambao sasa hivi upo nje ni kwasababu unafanyiwa matengenezo ya lazima na yanakaribia kukamilia na muda Si mrefu utarudishwa ili na wenyewe uanze kuzalisha”

“Nmewaelekeza Tanesco suala la kurudisha umeme mtu amekatiwa umeme MASAA 12 haitokubalika itokee anazidishiwa muda kurudishiwa umeme, umeme urudishwe kwa wakati na watu waendelee na shughuli zao mbalimbali” ameelekeza.

Aidha amewaelekeza Tanesco kuhakikisha matengenezo ya mitambo ya lazima yanafanyika kwa wakati na kwa muda mfupi ili kuendelea kuimarisha Hali ya upatikanaji wa umeme

Kapinga amewaelekeza TANESCO kuhakikisha inapotikea hitilafu, ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka ili umeme uendelee kupatikana

Pia amewaelekeza TANESCO kuendelea kuimarisha huduma kwa wateja, wahakikishe wanatatua changamoto za watanzania kwa wakati kwa kuimarisha mfumo wao wa utoaji huduma kwa wateja

“Hatutokubali wananchi walale giza kwa sababu ya umeme kusumbua na kutorekebishwa kwa wakati, waimarishe mifumo yao, waweze kufatilia na kuhakikisha wateja wanapata huduma kwa wakati pale wanapopata hitilafu”

Kadhalika Kapinga amewaelekeza Tanesco kuunganisha umeme kwa maeneo ambayo tayari Ina miundombinu.

“Sehemu ambayo kuna miundombinu ambayo Ina umeme na wananchi wameomba umeme, waunganishiwe umeme kwa wakati ili Kila mmoja aweze kufurahia huduma ya upatikanaji wa umeme”

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Mhandisi Isima Nyamhanga amesema kwa sasa shirika la TANESCO kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati wanafanya Kila juhudi zinazowezekana kuhakikisha kwamba kunakua na umeme wa kutosha kwenye gridi kwa kuweza kutumia kwaajili ya kuugawa kwa wananchi kwa shughuli za kijamii na kuzalisha mali.