January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Naibu Spika Zungu awataka madalali wa siasa waache kupita majimboni

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

NAIBU SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye ni Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu,amewataka madalali wa Siasa waache kupita majimbo ya wilaya ya Ilala bado yana wenyewe wapo madarakani waachwe wafanye kazi.

Mbunge Mussa Zungu, alisema hayo jimbo la Ukonga wilayani Ilala, katika mkutano mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala ambapo alialikwa mgeni rasmi.

“Ushindi wa chama cha Mapinduzi CCM upo Jumuiya ya Wazazi ya CCM ina wanachama wengi ndani ya Jumuiya ya Wazazi, ila kuna madalali wa siasa wanataka kumtoa Mbunge wetu wakati amefanya kazi kubwa za Serikali akiwa Wizara ya Ardhi na sasa amepewa Wizara mpya ya Habari tempe ushirikiano Mbunge wetu wa Ukonga Jery Silaa “alisema Zungu

Mbunge Zungu amewataka madalali wa kisiasa kuwaache Wabunge waliopo madarakani wafanye kazi zao mpaka muda ukifika ndio wafanye kampeni zao za kutaka majimbo kwa sasa muda wake bado .

Mbunge Mussa Zungu alisema kuwa ukiishi mbinguni usiope kupigwa ladi Chama cha Mapinduzi CCM ina jukumu kubwa sana ya kuwavusha Wenyeviti wa Serikali za mitaa ndio kazi iliyopo kwa sasa ili ccm ishike dola.

Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala inayoongozwa na Mwenyekiti wake Mohamed Msophe, kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na chama cha Mapinduzi na Serikali vizuri mpaka kufikia malengo yake.

Alisema awali Jumuiya ya Wazazi ilikuwa ina wanachama 20,000 kwa wanachama wamefikia elfu 60 000 ni kazi kubwa .

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala Mtiti Mbasa alitoa tamko la Jumuiya ya Wazazi CCM wilaya ya Ilala alisema wanampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kujenga nchi na kuleta maendeleo kwa wananchi wake ususani Wilayani Ilala.

Katibu Mtiti Mbasa ,alisema mikakati ya Jumuiya ya Wazazi wamejipanga kufanya ziara ya Matawi kila kata kwa ajili ya kutoa elimu ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa mwaka wa mwaka 2024 .

Alisema halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ina mitaa 159 CCM itashinda mitaa yote ya kata 36 kuwakikisha ccm ina shika dola na kuunda Serikali yake.

“Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Ilala tunaunga mkono utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM unaofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara pia tunamtakia maisha marefu Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ” alisema Mtiti.