Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
NAIBU Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Saady Khimji amegawa Futari kwa WAJANE na Watu wenye mahitaji Maalum wa Kata ya Ilala
Naibu Meya Khimji aligawa futari hiyo katika Ofisi ya Kata ya Ilala ambapo alikutana na WAJANE pamoja na makundi Maalum.
“Futari hii ambayo nimegawa Leo kwa ajili ya kuwapa Futari ndugu zangu Mwezi huu ni wa kupata Neema na fadhila za Mwenyezi Mungu”alisema Saady
Khimji alisema Futari hiyo aliyotoa kwa wananchi wake amepewa na wadau wake Shule ya FEZA International School mwakani atajipanga vizuri kwa ajili ya tukio kubwa kwani anajali mchango wa viongozi na makundi yote ambayo anashirikiana nao vizuri Katika kuleta maendeleo pamoja na kujenga Ilala.
Alisema amefarijika sana Katika jambo hilo kwa kushirikiana na KAMATI ya Maendeleo Kata na Wenyeviti wake wote.
Khimji aliwataka Wenyeviti wake wa SERIKALI za mitaa waendelee kushirikiana Katika utendaji wa kazi sambamba na kuleta maendeleo .
Aliwashukuru Wajane na Watu wenye mahitaji Maalum kuitikia wito wa kikao hicho Maalum cha kupokea Futari hiyo
Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa Ally Mshauri alimpongeza Diwani Saady Khimji kwa msaada huo kwa dhumuni la kuunganisha Watu wa Kata ya Ilala pamoja
Diwani wa Viti Maalum Wanawake Kata ya Ilala Asha Kipini alimpongeza Diwani Saady khimji kwa kugawa Futari hiyo pamoja na makundi maalum.
More Stories
Jokate awapa tano vijana UVCCM maandalizi Mkutano Mkuu wa CCM
Watakaokwamisha mapato Kaliua kukiona cha moto
Dkt.Gwajima aagiza kuundwa kamati za ulinzi wa watoto