Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Ilala
NAIBU Meya wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam,Ojambi Didas Masaburi ,amepewa uwanachama wa heshima na Umoja wa LITONGO Dar es Salaam (ULIDA)katika mkutano mkuu maalum wa umoja huo uliofanyika Jimbo la Kivule Wilayani Ilala ambapo mgeni rasmi alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara.
Akizungumza mara baada kupewa heshima hiyo Naibu Meya Ojambi Masaburi ,alisema atashirikiana na Umoja huo wa LITONGO kama mwanachama wa heshima ndani ya umoja huo ili uweze kuleta maendeleo na kukuza uchumi katika kuisaidia Serikali ya Tanzania ya uchumi wa viwanda.
“Ninashukuru heshima hii leo katika umoja huu tutashirikiana pamoja kwa niaba ya Serikali Mhe.Rais amesema tuviwezeshe vikundi hivi viweze kujikwamua na kukuza uchumi nitachangia milioni 10 na katika mkutano mkuu wa harambee yenu tutatafuta wadau kuwezesha kupatikana shilingi milioni 40 kwa ajili ya kununua uwanja wa kujenga shule kwa ajili ya mradi wa umoja wa Jumuiya yenu ya LITONGO Dar es Salaam ULIDA “alisema Masaburi
Naibu meya Masaburi alisema yeye ni Naibu Meya wa Halmashauri ya jiji kwa vipindi vinane alipongeza Umoja wa LITONGO ULIDA kuwa na mikakati ya maendeleo kwa ajili ya kuibua miradi ya maendeleo katika kukuza uchumi ili kuisaidia Serikali
Mbunge wa Tarime Vijijini Mwita Waitara ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo wa jamii ya watu wa Tarime alisema yeye taaluma yake mwalimu hivyo mikakati ya umoja huo wa kununua eneo la shule wanunue kuanzia hekari 10 ndio linatosha kwa kujenga shule .
Mbunge Waitara alipongeza uongozi wa umoja wa LITONGO Dar es Salaam ULIDA kwa kumpa cheti cha heshima umoja huo utafika mbali na anaendelea kuwasaidia jamii ya watu wa Tarime Vijijini kwa kuwa na yeye anatoka huko na wakati ukifika anaendelea kugombea katika jimbo la TARIME Vijijini kwa ajili ya kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutekeleza Ilani ya chama.
Wakati huohuo katika hatua nyingine Mbunge Waitara alisema viongozi watakaochaguliwa katika mkutano huo Kamati Tendaji amewapa mwaliko katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dodoma kwa ajili ya kufanya ziara.
Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Magdalena Thomas alichangia shilingi Milioni 1 umoja huo ili waweze kununua kiwanja cha shule huku mdau wa maendeleo Tarime akichangia shilingi Milioni tano.


More Stories
Kamishina TRA avitaka Viwanda viwili Mkuranga kulipa kodi inayostahili
Jimbo la Kibakwe wafanya ibada kuiombea nchi na viongozi wake
Wanafunzi Ilala Boma wafanya ziara ya Masomo uwanja wa ndege