Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Zuhura Yunus ametembelea Banda Jumuishi la Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar Es Salaam leo tarehe 5 Julai, 2024.
Aidha, amehimiza watumishi Ofisi ya Waziri Mkuu kuendelea kutatua changamoto za wananchi wanaotembelea banda hilo kwa ajili ya kupata huduma na uelewa masuala yanayotekelezwa na ofisi hiyo.
Katika Maonesho hayo Naibu Katibu Mkuu ametembelea Idara, Vitengo na Taasisi zilizopo chini ya ofisi hiyo kujionea namna huduma zinavyotolewa kwa wananchi na wadau wanaotembelea banda hilo katika maonesho hayo.
More Stories
UN yavutiwa na mkakati wa serikali wa utafiti wa madini nchini
Usaili wa walimu 201,707 wanaopigania ajira 14, 2025 sasa kufanyika  Januari 30
Marais wazidi kumiminika kuhudhuria mkutano wa nishati