March 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

NaCoNGO yazindua kikosi kazi cha ukusanyaji maoni

Na Penina Malundo,Timesmajira

BARAZA la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali(NaCoNGO),imezindua Kikosi kazi cha kitaifa cha wajumbe 14 ambao watakuwa na jukumu la kukusanya maoni ya wadau mbalimbali katika kufanya mapitio ya kanuni zinazosimamia baraza hilo.

Akiwatangaza wajumbe hao leo jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Baraza hilo,Gasper Makala amesema wajumbe wa kikosi kazi hicho ni kutoka katika makundi wakilishi mbalimbali ambacho kitafanya kazi kwa kushirikiana na wataalam kutoka kampuni ya Will Global.

Amesema Kamati hii itafanya kazi ya kukusanya maoni kwa wadau mbalimbali na kuhakikisha chochote kitakachokusanya kitakuwa shirikishi na kitakuwa na radha ya wanasekta ya NGo’s.

”Tunaushukuru Ubalozi wa Mataifa(EU) kwa kutuwezesha kupitia kanuni zinazosimamiwa na baraza hili,pia tunaishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia ushirikiano mkubwa tangu Baraza Jipya lilipoingia madarakani.

”Ikumbukwe kwamba Agost 28,2024 tuliwajulisha waandishi wa habari kuanza kwa zoezi hili,ambapo Februari 21,2025 tuliwatangazia umma kuwa leo ndio itakuwa siku rasmi ya kuzindua zoezi hili la ukusanyaji wa maoni chini ya kikosi kazi hicho,”amesema.

Ametaja majina ya wajumbe wa kikosi kazi hicho ambao wataongozwa na yeye Makala na wengine ni ni pamoja ⁠Adamson Nsimba ambaye ni Katibu Mkuu, NaCoNGO ,Prisca Ngweshemi ,Mweka Hazina wa NaCoNGO ,Joram Hongoli Mjumbe wa NaCoNGO ,Patrice Gwasma Mjumbe wa NaCoNGO ,⁠Edison Mwakyembe Mjumbe wa NaCoNGO .

Wengine ni ⁠Lupi Mwaisaka ni Mjumbe wa NaCoNGO, ⁠Francisca Damian Mjumbe wa NaCoNGO Vijana , Advocate Mariam Othman ni Mkurugenzi Mtendeni TLS, ⁠⁠Dkt.Riziki Nyello Mhadhiri Institute of Social Work,Dkt.Astronaut Bagile Mkurugenzi Kampuni ya WISE, ⁠Advocate Gloria Mafole kutoka CCT, Asina Shenduli kutoka Baraza la Waislamu Tanzania( BAKWATA ) pamoja na ⁠Edmund Matotay kutoka Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).

Makala amesema pia kikosi hicho kitashirikiana na wataalam kutoka kampuni ya Will Global ambao ni Henry Muguzina kusaidiwa na Bubezwa kaiza.”Tutafanya mapitio ya kanuni zinazosimamia na baraza hilo za Mwaka 2016,Tutafanya mapitio ya kanuni za uchaguzi wa baraza za NaCoNGO za Mwaka 2016 na tutafanya mapitio ya mkakati wa mpito ya baraza hilo ili kuboresha mkakati mpitio,”amesema.

Kwa upande Meneja wa Asasi za Kiraia kutoka Umoja wa Ulaya(EU),Neema Bwaira amesema Umoja wa ulaya ni mdau mkubwa wa maendeleo nchini Tanzania kwani wanafanya kazi na waadau mbalimbali ikiwemo Serikali na Asasi za Kiraia.

Amesema kupitia zoezi hilo linalofanywa na Baraza la NaCoNGO wameona kuna umuhimu wa kushirikiana na kufanya kazi na baraza hilo ili kuweza kuboresha mazingira ya utendaji kazi wa Asasi za Kiraia Tanzania.

”Sisi kama wadau maendeleo tunawatakia mchakato mwema ambao utakwenda kukusanya maoni na kupitia kanuni kama zilivyoainishwa pamoja na kuuisha Mpango mkakati wa NaCoNGO utakaoweza kuhakisi mambo mbalimbali.

”Tunaaamini kazi yote itakayofanyika itakuwa kwa manufaa ya sekta za Asasi ya kiraia Tanzania na maendeleo ya nchi ya Tanzania na wananchi kwa ujumla,”amesema