January 4, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Nabii Suguye aongoza uchangiaji damu

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Kufuatia siku ya wafanyakazi Duniani katika kuungana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kanisa la WRM linaloongozwa na nabii Nicholaus Suguye limeshiriki zoezi la uchangiaji damu, upandaji miti sambamba na kutoa vifaa vya matibabu kwa wagonjwa wa hospital ya wilaya ya kivule iliyopo kivule.

Zoezi hilo likiongozwa na mtumishi wa mungu nabii nicholaus suguye viongozi mbalimbali wa kanisa hilo pamoja na waumini ambapo nabii suguye amefafanua kwa kina kwa nini wameamua kufanya hivo ikiwa ni sehemu ya ushiriki wao kwa jamii ya kivule lakini kurudisha matumaini kwa wagonjwa na kuungana na serikali katika kuisaidia jamii.

Nabii suguye pia ametoa pongezi kwa majengo ya kisasa yaliyopo katika hospitali ya wilaya ya Ilala na kutoa wito kwa wadau mbalimbali kushirikiana na serikali katika kuisadia jamii.

Naye mganga mfawidhi wa hospital ya wilaya ya ilala dr nyamboto thobias ametoa shukrani na kuelezea namna walivyofarijika na msaada huo walioupokea huku akiahidi vifaa hivyo vitakwenda kuwasaidia wagonjwa katika hospitali hiyo.

Nao baadhi ya walioshiriki katika shughuli ya usafi na upandaji miti na kuchangia damu mwinjilisti mkuu Ana suguye anaeleza umuhimu wa zoezi hilo pamoja na washiriki mbalimbali kuwa litasaidia utunzaji wa mazingira pamoja na kivuli.

Kwa upande wa wagonjwa na wahudumu wa hospital ya ilala wametoa pongezi huku wakimshukuru nabii suguye kwa kuwakumbuka na kutoa wito kwa wengine wanaoguswa kujitokeza na kuchangia damu na vifaa.

Kauli mbiu katika zoezi hilo ni mungu usafi na afya ambapo kanisa la wrm wametoa giving set infusion pc 500, jik au bleech litre 25 sabuni za maji litre 25 syring boz 40 ambapo kwa sasa hospital hyo ina majengo 13 yaliyokamilika ikihudumia wagonjwa 200 kwa siku wa kutwa na kulazwa huku majengo mengine yakiendelea na ujenzi.