September 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwila ataka Ngoma za unyago zifuate maadili kwa vijana

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM Kata ya CHANIKA William Mwila, amewataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa wasimamie Ngoma za Unyago zifuate maadili zisiaharibu vijana ni Taifa la kesho.

Mwenyekiti wa ccm Chanika William Mwila ,alisema hayo katika kilele cha madhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika Dunia kata ya CHANIKA yalioandaliwa na Fahari Tuamke Maendeleo.

“Tunawaomba Wenyeviti wa Serikali za mitaa ambao mnatoa vibari ngoma za unyago zifuate maadili katika mitaa yenu ili watoto wasiingie katika mmomonyoko wa maadili Serikali inategemea vijana kwa ajili ya Taifa la kesho hivyo vijana wa walindwe”alisema Mwila

Mwenyekiti Mwila ,aliwataka Wenyeviti wa mitaa kutoa vibari na kuzitaka ngoma za unyago kupiga katika sehemu maalum na kuzitaka kufuata maadili ya nchi yetu ili vijana wasiingie katika mmomonyoko wa maadili na makundi yasiofaa.

Alisema Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa vipaumbele vyake katika sekta elimu msingi mpaka elimu Sekondari zote bure na Chuo wanatoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi hivyo vijana amewataka wasome kwa bidii na kuzingatia masomo .

Aliwataka Wazazi watimize wajibu wao watoto wawezeshwe kupata elimu bora mpaka chuo kikuu Serikali inategemea vijana kwa ajili ya Taifa la kesho ili Taifa liwe bora watu wake wanatakiwa wasome.

Aidha aliwataka Walimu wafanye kazi kwa bidii kwa ajili ya kutimiza wajibu wao na malengo ya Serikali .

Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau ,alisema Fahari Tuamke Maendeleo wameadhimisha siku leo ya Mtoto wa Afrika kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam katika maadhimisho hayo .

Mwenyekiti wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau alisema kauli mbiu ya Mwaka huu siku ya mtoto wa Afrika Elimu Jumuishi kwa watoto izingatie Maarifa na Stadi za Kazi elimu Jumuishi ina elekeza watoto wasibaguliwe wapatiwe elimu bora na elimu Jumuishi

Alisema Fahari Day Care inaunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kuwekeza sekta ya Elimu na kutoa elimu bora ili iweze kutoa elimu bora ili waweze kulea jamii bora wasiingie katika mmomonyoko wa maadili