November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwera aeleza mafanikio yake

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa vikongoro Seif Mwera ,aeleza Mafanikio ya utekelezaji wa Ilani kwa kipindi cha uongozi wake zikiwemo ujenzi wa Barabara za mitaa ,shule za Msingi ,umeme wa REA vivuko vya Barabara .

Aidha Mwenyekiti Mwera kipindi cha uongozi wake pia mwaka alipata pesa za mfuko wa jimbo kwa ajili ya kivuko shilingi milioni 1.5 ufadhili wa mradi wa Maji salama uliofadhiliwa na SOS ambapo kwa sasa Mradi huo unasimamiwa na DAWASA.

” Diwani aliatatua kero ya umeme katika maeneo ya chambala ,Manzese Mwanambong’o umeme wa REA ulipatikana kwa wananchi wote walioomba ,ujenzi wa vikuko.kimoja kwa Kisungula kupitia mfuko wa jimbo,kwa Matumbo kupitia PWT TASAF mfuko wa Jimbo kivuko cha shilingi milioni 1.5 alisema Mwera.

Mwenyekiti Seif Mwera alisema pia ujenzi wa nyumba tano za watu wasio na makazi bora unajengwa na HABITAT kwa kushirikiana na TAWA kwa usimamizi wa Halmashauri na Serikali kuu,uundwaji wa Kamati za Wazee ,usajili wa vikundi vya Bodaboda mradi wa upandaji wa miti ya mbao kupitia PWP na TASAF.

Alisema katika zoezi la urasimishaji jumla ya wakazi 4367 wote walirasimishiwa maeneo yao vikongoro yote viwanja 1100 vilipandwa mawe viwanja vilivyosajiliwa 670 viwanja vilivyopata hati miliki 501 .

Akizungumzia miundombinu ya eneo hilo alisema changamoto baadhi ya Barabara za ndani ambapo utatuzi wake unatarajia kumalizika hivi karibu Serikali itaanza ujenzi wa barabara hizo .

Alipongeza Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani kwa vitendo amewataka wananchi kuunga mkono juhudi za Serikali yetu ambayo imewekeza katika sekta ya Elimu msingi Elimu Sekondari sekta ya afya kwa kujenga shule nyingi na vituo vya afya .

Pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jery Silaa na Diwani wa Kata ya CHANIKA Wilayani OJAMBI MASABURI kwa kuleta maendeleo ya wananchi na kusimamia Ilani vizuri CHANIKA sasa imepata maendeleo makubwa na fursa za kiuchumi.

.Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Ilala Mwinyimkuu Sangaraza aliwataka vijana kufanya kazi ili kukuza uchumi wa nchi yao badala yake wasikae vijiweni kushindwa kufanya kazi baadae wailaumu Serikali kwa kushindwa kupata kipato.