Na Rose Itono Bagamoyo
MWENYEKITI wa JUMUIYA ya Wazazi Chama Cha Mapinduzi ( CCM) Kata ya Zinga Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, Hassan Kashingo amesema Kata hiyo Ina mikakati ya kuhakikisha Kila tawi ndani ya Kata yake linapata mtajii ili kuweza kujikwamua kiuchumi
Akizungumza kwenye Maadhimisho ya wiki ya wazazi wilayani hapo iliyoambatana na shughuli mbalimbali za kimaendeleo ikiwepo zoezi la upandaji niti Kashingo amesema ili wananchi wa kata hiyo waweze kujikwanua kiuchumi atahakikisha kila tawi linapata mtaji wa kuanzisha shughuli. zao za kujipatia kipato
Amesema katika Maadhimisho ya wiki ya wazazi wilayani hapo kata yake imeweza kuzindua Kigoda Cha Wazazi Shina la Kibururu kilichopo ndani ya Kata hiyo ili kuweza kuwaweka wanachama pamoja na kujadili mambo ya msingi zikiwepo shughuli za kiuchumi
Pia imeweza kuzindua Duka la Wazazi ambalo litawezesha kuendesha shughuli za kiuchumi kupitia bidhaa zitakazouzwa.
Kashingo amesema ndani ya wiki hii ya Wazazi kiwilaya wameweza kupanda miti 500 katika Kata ya Zinga ili kurudisha uoto wa asili.
“Tumefanikiwa kupanda miti zaidi ya 500 ,katika eneo la mnada lililopo kwa Mtoro Kata ya Zinga ili kuweza kurudisha uoto wa asili uliopotea kutokana na vitendo Vya baadhi ya watu kukata miti hovyo,” amesema Kashingo

Mwenyekiti pia ameahidi kuhakikisha anatumia nguvu yake na ajili kuhakikisha anaisimamia na kuilinda miti hiyo kwa kushirikiana na wananchi wake ili kuweza kuwa na uchumi wa bluu kwenye eneo hilo
“Katika kutekeleza agizo la Rais Dkt. Samia Suluhu Hasana la kutunza na kuhifadhi mazingira nitahakikisha miti iliyopandwa eneo la mnadani lililopo ndani ya Kata yangu inakua na kurudisha uoto wa asili uliopotea pamoja na kupambana na wimbi la na ukataji wa miti hovyo ambao unasabisha hali ya ukame,” amesema

Naye Mkuu wa Kitengo cha Maliasili na Mazingira katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoto Dkt. Obed Mwinuka amebainisha kwamba lengo lao kubwa ni kutekeleza kampeni ya kitaifa katika kuboresha mazingira ambapo wamefanikiwa kupanda miti ipatayo 500 katika eneo hilo la mnada wa mbuzi na ng’ombe lililopo kata ya Zinga.
More Stories
BAKWATA yawazawadia washindi wakuhifadhi Qur’an
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya