November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi, ahukumiwa kifungo jela

Na Mohamed Hamad,TimesMajira Online,Kiteto

MWENYEKITI wa Baraza la Ardhi Kata ya Bwawani Wilayani Kiteto mkoani Manyara, Steven Tadayo amepatikana na hatia ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na sheria.

Akisoma Hukumu hiyo Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Kiteto, Mossy Sasi amesema mahakama iomeona kuwa mshtakiwa ambaye ni mwenyekiti ana kosa la kuomba na kupokea Rushwa.

Hakimu Sasi akitoa hukumu hiyo alisema mtuhumiwa anatakiwa kulipa faini ya sh. 500,000 kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha Miaka mitatu (3) Jela.

Hata hivyo katika maamuzi hayo mshtakiwa wa pili Maiko Robert Lemabi ambaye alikuwa Katibu wa Baraza hilo ameachiwa huru.

Pia Mahakama imeamuru mwenyekiti huyo wa Baraza kurejesha fedha za Rushwa TAKUKURU ambazo alizipokea kwa njia mtandao wa simu.

Mapema Julai 2019 washtakiwa hao walimweleza mwananchi mmoja kuwa kufungua shauri anatakiwa kulipa kiasi cha sh.10,000 ikiwa ni gharama ya Baraza. Sanjari na gharama halali walimtaka mwananchi huyo awape sh.20,000 (Rushwa) ndio wafungue shauri hilo.

Kesi hiyo ya jinai ilikuwa inaendeshwa na Wakili Yahaya Masakilija wa TAKUKURU na baada ya hukumu amesema amepokea uamuzi huo wa Mahakama.