January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti wa ACT, aongoza kikao cha chama

Na Mwandisi Wetu, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa ACT- Wazalendo Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, leo Agosti 24, 2024 ameshiriki na kuongoza Kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho.

Othman amekiongoza kikao hicho katika Ukumbi wa Hakainde Hichelema, uliopo katika Jengo la Maalim Seif, ilipo Makao Makuu ya ACT-Wazalendo, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Othman yupo jijini Dar es Salaam, kwaajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu inayohusisha shughuli mbali mbali za serikali, jamii na siasa.

Viongozi mbali mbali wameshiriki katika kikao hicho wakiwemo, Kiongozi wa Chama, Doroth Semu; Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Zanzibar, pamoja na wa upande wa Tanzania Bara, Ismail Jussa, na Is-haka Mchinjita; Kiongozi wa Chama Mstaafu, Zitto Kabwe; na Mwenyekiti Mstaafu, ‘Babu’ Juma Duni Haji.

Kikao hicho ni cha kwanza kwa-mujibu wa katiba, tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu wa ACT-Wazalendo, mapema Machi, 2024.