January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti TEF amshukuru Rais Samia kuona umuhimu wa kupitia sheria ya habari

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MWENYEKITI wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu kwa kuona umuhimu wa kupitia sheria za habari na kuagiza zifanyiwe maboreshio ili kuendana na mazingira yaliyopo.

Balile ameyasema hayo alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Clouds TV tarehe 28 Julai 2022 Jijini Dar es Salaam.

Pia Balile amemkumbusha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuongeza kasi katika mchakato wa mabadiliko wa sheria ya habari nchini lengo kuondoa baadhi vipengele vya sheria hiyo ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wadau wa habari nchni kwa kuminya uhuru wa vyombo vya habari.

Balile amebainisha kuwa endapo mchakato huo wa mabadiliko ya sheria ukikamilika utaleta uhuru wa habari hapa nchni bila kuumiza mwengine.

“Tufahamu kuwa uhuru wa habari ni haki ya msingi ambayo wengi wanaitaka. Vyombo vya habari visipokuwa huru, wananchi nao pia wanakosa uhuru ikiwa ni pamoja na kutoa maoni yao pia kupata taarifa zinazowahusu moja kwa moja,” amesema.

“Tunapozungumzia uhuru wa vyombo vya habari, sio kwamba tunataka upendeleo kutoka serikalini, la! Tunacholenga hapo kila mmoja apate haki na awajibike,” ameonge