November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti Sidde amewataka CCM Mnyamani kujipanga kushika Dola

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Al haj Said Sidde , amewataka wana CCM Mnyamani kujipanga kwa ajili ya kushika Dola 2024 Uchaguzi wa serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025 wa Rais, Wabunge na madiwani .

Mwenyekiti Said Sidde aliyasema hayo Kata ya Mnyamani wakati Diwani wa Mnyamani Shukuru Dege, alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani .

“Wana CCM wa Kata ya Mnyamani sasa tunaenda katika vita tujipange Ili chama chetu kiweze kuendelea kushika Dola chaguzi za Mitaa na Uchaguzi Mkuu,Sasa tufanye kazi za chama ndani ya chama na nje ya chama ” alisema Sidde .

Aliwataka Viongozi wa CCM kutangaza mambo mema yanayofanywa na serikali yetu katika utekezaji wa Ilani, Mnyamani ya sasa ipo salama aliwasisitiza wajenge mahusiano ya chama na serikali,Pia aliwapongeza viongozi wa Kata na matawi Kwa kujituma kwao kufanya kazi za Chama

Wakati huohuo aliwataka wajaze safu za viongozi wa CCM ngazi ya Matawi na Kata sambamba na kuwatoa WALIOSHINDWA kufanya kazi za chama kuweka wengine Ili kazi ziendelee, kwani sasa wasiofanya kazi hawana nafasi,Huu ni muda wa kujenga chama,

Katika hatua nyingine aliwataka umoja wa Vijana UVCCM kujipanga na kuonyesha makucha yao ndani ya chama na jumuiya,

DIWANI wa Mnyamani Shukuru Dege, aliezea mafanikio ya Mnyamani ambapo alimpongeza Mbunge wa Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kwani amempa ushirikiano mkubwa katika kutatua Changamoto za Kata ya Mnyamani,Pia ameipongeza serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta Maendeleo ambapo kata ya Mnyamani Serikali imewapa shilingi milioni 150 kwa ajili ya shule ya Msingi ya Kisasa

Diwani Shukuru Dege alisema mafanikio mengine Kata ya Mnyaman ni pamoja na shilingi milioni 500 zimetengwa kwa ajili ya barabara za ndani Ili Miundombinu iweze kupitika kwa urahisi.

DIWANI Shukuru Dege ameshauri Halmashauri ya jiji kulipa Fidia kwa wakati Ili UJENZI wa shule uweze kuwanza kwa wakati Wanafunzi wasome

Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto alisema atakikisha pesa zote za maendeleo zilizoelekezwa Mnyamani zitaelekezwa zikiwemo za Afya ,Miundombinu,Bajeti ya barabara ya Faru itaelekezwa Ili barabara ijengwe ,aliwataka Wananchi waliokopa Mikopo ya serikali inayotolewa ngazi ya Halmashauri kulipa kwa wakati Ili ziweze kutumika kusukuma maendeleo .

MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi Mnyamani Mbaraka Mwinyimvua ameishukuru serikali ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kukiboresha kituo Cha Afya Mnyamani,kutenga Ofisi ya kata ya kisasa na sasa wanaenda kujenga Shule na Barabara
Amempongeza Mbunge Bonnah Kamoli, kwa kuendelea kutatua kero ambao kwa Sasa Kupitia mfuko wa Jimbo wameipa Mnyamani fedha kwa ajili ya ununuzi wa samani za ofisi ya Mtendaji wa Kata

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said SIDDE Akizungumza na Viongozi wa CCM kata ya Mnyamani wakati Diwani wa Mnyamani Shukuru Dege alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa ILANI Machi 20/2023
(aliyekaa)Mwenyekiti wa CCM Mnyamani Mbaraka Mwinyimvua
Mwenyekiti wa chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Mnyamani Mbaraka Mwinyimvua akizungumza katika mkutano wa Halmashauri kuu wakati Machi 20/2023 Diwani Shukuru Dege alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani (aliyekaa )Mwenyekiti wa CCM Wilaya Said Sidde.
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde akikabidhi kadi za CCM Kwa wanachama wapya Buguruni Mnyamani wakati Diwani Shukuru Dege alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani Machi 20/2023.
Diwani wa Kata ya Mnyamani Shukuru Dege akisoma Taarifa ya Utekelezaji wa ILANI ya ccm Machi 20/2023.
Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto akizungumza katika mkutano wa Halmashauri kuu Buguruni Mnyamani wakati Diwani shukuru Dege alipokuwa akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa ILANI Machi 20/2023