Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Ilala Sabry Abdalah Sharif, ameongoza wiki ya JUMUIYA ya Wazazi kata ya Ilala kwa kupanda miti ya Matunda na vivuli.
Mwenyekiti Sabry Abdalah Sharif, aliongoza kampeni hiyo ya kupanda miti leo kata ya Ilala na matawi yake yote kwa kushirikiana na Kamati ya Utekelezaji ya kata ya Ilala.
Akizindua kampeni ya kupanda miti Ilala Mwenyekiti Sabry alisema katika madhimisho ya kupanda miti ILALA ndani ya kata Ilala walipanda miti hiyo mitaa yote minne katika Barabara za kisasa za Serikali .
“Tunaunga mkono juhudi za chama cha Mapinduzi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, katika sekta ya mazingira na suala zima la kutunza mazingira na sisi Jumuiya ya Wazazi ILALA tunasimamia sekta ya Elimu, Afya na Mazingira “alisema Sabry.
Alisema kilele cha wiki ya Jumuiya ya Wazazi mwaka huu yanatarajia kufanyika Mkoani Mwanza Kitaifa hivyo aliziomba jumuiya zake za matawi kuendelea kupanda miti na kufanya kazi za kijamii na za jumuiya ya Wazazi.
Aidha aliwataka Wazazi wa kata ya Ilala kila kaya kupanda miti mitano kama sehemu ya utunzaji wa mazingira na kuifadhi vyanzo vya maji ili nchi yetu isigeuke kuwa jangwa.
More Stories
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni