January 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenyekiti CCM Ilemela ashiriki uchimbaji msingi Kawekamo

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

Katika kuhakikisha ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kilimani Kata ya Kawekamo unakamilika kwa wakati, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Ilemela Yusuph Bujiku ameshiriki zoezi la uchimbaji wa msingi.

Ambapo Mwenyekiti huyo wa CCM Wilaya ya Ilemela ameungana na wananchi,viongozi mbalimbali pamoja na wadau wa maendeleo wa Kata hiyo katika zoezi hilo lililofanyika Oktoba 13,2022.

Akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kawekamo Bujiku,amewashukuru wananchi kwa kujitoa kwao katika shughuli za kijamii kwani inachangia kuleta maendeleo na kukamilisha miradi kwa haraka.

Pia amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya naendeleo katika sekta ya elimu ambapo Ilemela ilipata kiasi cha bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 110 katika shule za sekondari.

“Shule ya sekondari Kilimani imepata mgao wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 3,haya ni matunda ya kuwa na Rais mwenye maono na mwenye kujali sekta ya elimu,”ameeleza Bujiku.

Hata hivyo ujenzi huo wa vyumba vya madarasa m ni maandalizi kwa ajili ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela Yusuph Bujiku (mwenyewe kofia ya kijani) akiwa na baadhi ya wananchi wakati wa zoezi la uchimbaji wa msingi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Kilimani Kata ya Kawekamo.