December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenge yapitia miradi ya Sh. Bil 1.4 Halmashauri ya Wilaya Mbulu

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mbulu

Jumla ya Miradi 5 yenye thamani ya sh.bil.1,489,355,707 ilipitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.

Hayo yalibainishwa juzi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbulu Mkoani Manyara Abubakar Kuuli wakati alipokua akitoa taarifa ya miradi mbele ya Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2022 Sahili Geraruma, Mkuu wa wilaya hiyo Sezaria Makota wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mbulu katika eneo la Tlawi.

Kuuli alisema Mwenge wa Uhuru ulipokua katika halmashauri ya wilaya ya Mbulu ulifanikiwa kutembelea miradi mitano (5) yenye thamani ya sh.bil.1.4

” Mradi wa kwanza kabisa kufikiwa Mwenge wetu wa Uhuru ni mradi wa vyumba vitatu vya madarasa ( sekta ya elimu ) ambavyo zilizinduliwa na mbio hizi za mwenge, mradi ulipo katika Kata ya Geterer uliogharimu sh.mil.62,190,357.

Aidha alisema mradi huo ni fedha kutoka serikali kuu sh.mil.60, huku Halmashauri mayo ilkichangia jumla ya sh.mil2,190,357, katika Kata ya Haydom Mwenge wa Uhuru ulitembelea kuona na kukagua kikundi cha kutengeneza chaki ( MECOG ) ambacho kinafanya kazi, wananchi waliweza kukichangia kikundi hiko jumla ya sh.mil.6,075,000 huku Halmashauri nayo ikitoa sh.mil.10,925,000″ alisema Kuuli.

Mradi mwingine uliopitiwa na Mwenge wa Uhuru na kuweka jiwe la Msingi ni mradi wa ujenzi wa barabara ambao unaendelea uliogharimu sh.mil. 299,573,000, ujenzi wa mradi wa Maji ambao inaendelea pia uliwekewa jiwe la Msingi, pia Mwenge ulipitia kituo cha afya.

Aidha Mkurugezni Kuuli alifafanua kuwa Kati ya hizo fedha zote za miradi wananchi walichangia sh.mil.6,075,000, serikali kuu sh.bil.1,470,165,350.