January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenge wazindua shule Mpya Mkoani Manyara

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Mbulu

Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 umezindua Shule Mpya ya Msingi Flatei Massay iliyopo Kijiji na Kata ya Haydom Katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara, huku Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim akiwapongeza viongozi wa Wialya hiyo ikiongezwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Kheri James, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Abubakar Kuuli, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Joseph Mandoo pamoja na Mbunge wa Jimbo hilo Flatei Massay Kwa uwajibikaji wao, ikiwa ni sambamba na kusimamia miradi hiyo kikamilifu.

Kaimu ameyasema hayo juzi alipokua akizungumza wakati akikagua shule nankisha kuzindua mradi huo, ambapo amesema kuwa ni mradi mzuri utakaowasaidia wanafunzi kuondoka na acha ya kute!Bea umbali mrefu kufuata shule.

Aidha Kaim amefafanua kuwa ni vema Sasa wanafunzi wakatambua u!uhimu wa miundombinu hiyo kuwa imetumia gharama kubwa kugharamia Ujenzi wa shule, hivyo wanatakiwa kujilinda miundombinu hiyo ili nayo ije iwatunze kizazi na kizazi.

“Ndugu zangu niwapongeze viongozi wetu wote Kwa juhudi mbalimbali katika kuhakikisha mrdi huu unakamilika na ili kuweza kuharakisha kutoa huduma kwa watoto wetu ambao Leo hii tunafurahi mradi umekamilika, utunzeni huu mradi, kama mlivyosikia Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan ameleta fedha nyingi hapa na shule imekamilika” amesema Kaim.

Akisoma taarifa ya mradi huo mbele ya Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdalla Shaib Kaim, Mwl. Mkuu wa Shule ya Msingi Haydom Joshua John Mwambo amesema Shule hiyo ni ya mkondo mmoja wenye vyumba 9 vya madarasa, Jengo la Utawala, vyoo ya matundu 16 na kichomea taka.

Mwl. Mwambo amesema shule mpya ya Msingi Flatei Massay ilipokea fedha jumla ya sh.kil.348,500,000 kutoka Serikali kuu kupitia mradi wa Boost.

” Fedha za Ujenzi wa mradi huu zilipokelewa mnamo April 24, 2023, Kisha mradi ukaanza kutekelezwa Mei 30,2023 na kukamilika mnamo Septemba 30, 2023, mradi huu umetekelezwa Kwa mfumo wa force account ” amesema
Mwl.Mwambo.

Aidha amesema hadi kukamilika Kwa mradi huo umegharimu jumla ya sh.mil.366, kati ya fedha hizo wananchi wamechangia jumla ya sh.mil.17.5, huku Serikali kuu ikichangia sh.mil.348.5.

Akielezea mafanikio ya mradi amesema ni pamoja na kuondoa msongamano wa wanafunzi darasani, kuboresha Mazingira ya kufundishia na kujifunzia, kuongezeka kwa imani ya wananchi Kwa Serikali yao, na hivyo wananchi kuhamasika kuchangia miradi mbalimbali nankutunza miundombinu ya shule.

Kufuatia Ujenzi wa shule kama kichocheo kikubwa cha upatikanaji wa elimu katika Kijiji na kata ya Haydom, wananchi wamemshukuru Rais Dkt.Samia Suhulu Kwa kuwapatia fedha Kwa ajili ya Ujenzi huo wa shule.

” Kama inavyofahamika Taifa lolote lile duniani linapokosa elimu ni lazima litatawaliwa na umaskini, hivyo kitecho cha Rais Samia Suluhu Hassan kuwapatia fedha ni uzalendo mkubwa, wa kuwataka wananchi wale wasome ili waondoe ujinga.

” Hata Hayatinbaba wa Taifa Mwl.Julius Kambarage Nyerere alituambia wazi kuwa maadui watatu wa kukabiliana nanumaskini Moja wapo ni Ujinga, huku pia maandiko ya dini nayo hayakutuacha nayo yametutaka amanyanasema ” Mshike sana elimu, usiniache aende zake ” hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu kwa fedha za mradi huu wa shule” amesema.

Naye Mbunge wa jimbo la Mbulu Vijiji Flatei Massay ameipongeza Rais Dkt.Samia wa kuwapatia za Kwa ajili ya Ujenzi wa shule hiyo ni Mkombozi wa Kijiji cha Haydom.

Hata hivyo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023 abdalla Shaib Kaim amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Kheri James pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Abubakar Kuuli kwa uwajibikaji wao katika kusimamia shughuli mbalimbali za Maendeleo ikiwa ni pamoja na kusimamia kikamilifu miradi iliyipitiwa na mbizo za Mwenge wa Uhuru 2023.