Na heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
MWENGE wa Uhuru umeweka jiwe la Msingi Kituo cha AFYA Kata ya Kipunguni Wilayani Ilala.
Katika uzinduzi huo wa kuweka jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2022 SAHILI NYANZABARA, alipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Samia Suluhu Hassan ,kwa kujenga vituo vya Afya vipya nchi nzima kwa kutumia pesa za Miamala ya simu (TOZO).
Kiongozi wa Mwenge NYANZABARA alisema mradi huo wa kituo cha Afya ambao umetumia fedha za Miamala ya simu (tozo) ukikamilika Jamii ya Kata ya Kipunguni watanufaika na Mradi huo mkubwa pamoja na maeneo ya jirani.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala Dkt.Elizabeth Nyema alisema kituo cha Afya Kipunguni kimegharimu shilingi milioni 250 pesa za Miamala ya simu (TOZO) za Serikali kwa Sasa ujenzi wake umefikia hatua za umaliziaji kwa majengo ya wagonjwa wa nje na Maabara na pindi kitakapo kamilika kabisa huduma zitaanza kutolewa.
Mpango unaofuata ni kujenga kichomeataka, jengo la mama na mtoto na jengo la upasuaji ili kuongeza huduma na kupunguza rufaa kwa wagonjwa.
DIWANI wa kata ya Kipunguni Wilayani Ilala ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Huduma za Jamii Jiji la Dsm, Stephen Mushi, alimpongeza sana Rais wa Jamhuri ya MUUNGANO wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,Mbunge wa Jimbo la Ukonga Jerry Silaa kwa kuelekeza fedha za vituo vya afya Wilaya ya Ilala ambapo Kata ya Kipunguni imenufaika na Ujenzi wa Kituo cha AFYA kitakachotumika na wakazi zaidi ya 32,000.
DIWANI Mushi alisema ni Historia kwa mara ya kwanza kwa Mwenge Wa Uhuru Kufika na kuweka Jiwe la msingi.
Kata ya Kipunguni ina mitaa minne ambayo ni Kipunguni B,Kitinye, Machimbo na Amani Wananchi wake wote watanufaika na Kituo hicho cha afya Cha kisasa Mushi alisema kwa Wilaya ya Ilala kituo hicho ni cha mfano ni sehemu ya Utekelezaji wa Ilani ya chama Cha Mapinduzi CCM ametekeleza Moja ahadi yake kubwa kwa Wananchi wake wa Kata hiyo Wakati alipokuwa akiomba kura alitoa ahadi ya kujenga kituo cha AFYA katika uongozi wake wa Udiwani.
More Stories
Makalla:Kupanga fujo ni dalili za kushindwa uchaguzi
Tanzania yapanda viwango Utawala wa Sheria Duniani
Rais Samia apeleka neema Tabora