December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenezi Makonda akabidhi magari 2 ya kubebea wagonjwa

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda amekabidhi Magari mawili (2) ya kubebea wagonjwa kwa Wilaya ya Bagamoyo na Chalinze Mkoani Pwani.

Mwenezi Makonda amekabidhi magari hayo Jana tarehe 19 Januari, 2024 kabla ya kuzungumza na Wananchi wa Pwani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Bagamoyo.

Magari haya ni ukombozi mkubwa kwa wanawake wa Tanzanja katika kupata huduma za Afya kwa haraka na hii ndio dhamira ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ” Alisema Mwenezi Makonda

Naye, Waziri wa TAMISEMI Mchengerwa amesema kuwa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuendeleza jitihada za kuboresha miundombinu katika sekta ya afya alitoa takriban Bilion Tsh 52 na imetumika kununua magari 528 na magali 332 ni ya kuhudumia wagonjwa, 212 sekta ya afya na kubainisha kuwa hii ni mara ya kwanza katika historia serikali ya Tanzania imenunua kwa fedha zake.