January 24, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda amesema siku ya Shukrani kwa Mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua na kuwashukuru Walipakodi wote wakubwa na wadogo.

Amesema utoaji wa tuzo ni kutambua Walipakodi waliyofanya vizuri katika sekta mbalimbali zikiwemo sekta ya Madini, Taasisi za Umma, Taasisi za Fedha, Sekta ya uzalishaji na Viwanda, Sekta ya Utalii, Walipakodi wakubwa na Tuzo ya Kamishna Mkuu.

Kamishna Mkuu Mwenda amevitaja vigezo vitano vilivyotumika kuwapata washindi wa tuzo kuwa ni Mlipakodi mwenye rekodi nzuri katika ulipaji wa Kodi, Mlipakodi anayelipa kwa hiari na kwa wakati, Mlipakodi anayetumia EFD mashine na VFD kikamilifu, Mlipakodi aliyelipa kodi kubwa zaidi na Mlipakodi anayetoa ushirikiano kwa TRA.

Amesema wapo washindi waliofanikisha makusanyo makubwa ya Kodi katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/2025 ambapo TRA ilivuka malengo kwa kukusanya Sh. Trilion 16.528 ambao pia watatunukiwa.

“Mimi na wenzangu ndani ya TRA Tutaendelea kutekeleza maagizo yako yote, Tutaendelea kupambana na wanaofanya magendo, Tutaendelea kukusanya Kodi kwa kiwango kikubwa bila kuwa na migongano na Walipakodi, Tutaendelea kutatua migogoro na kuwasikiliza Walipakodi, Tutaendelea kutoa huduma Bora” Kamishna Mkuu Mwenda