Na Hadija Bagasha Tanga.
WAWEKEZAJI wa viwanda Mkoani Tanga wameishukuru serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na sera yake ya viwanda ambayo imewasaidia wawekezaji wengi kupata msaada pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali na hivyo kusaidia kupata moyo wa kuendelea kufanya kazi kwa ufanisi zaidi licha ya kukabiliwa na baadhi ya changamoto mbalimbali ikiwemo kukatika kwa umeme ambayo imekuwa ikiwasababishia hasara.
Pongezi hizo zimetolewa na mwekezaji wa kiwanda cha kuzalisha gesi ya oksijeni cha jijini Tanga
cha Open Oxijen Product East Africa Ltd, Mohammed Said Abanoor wakati akizungumza na kituo hiki wakati wa maonyesho ya 9 ya biashara na, utalii yanayofanyika jijini Tanga.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba hatua hiyo inatokana na wasaidizi wa Rais akiwemo mkuu wa mkoa ambapo wamekuwa wakiwatembelea mara kwa mara kwajili ya kuwatia moyo na kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo.
Aidha alisema kitendo hicho kinawapa faraja kubwa na kuona serikali yao inawajali na kuwathamini jambo ambalo linapelekea kufikiria namna ya kupanua wigo wa uzalishaji ambao utaleta tija kwao na watanzania kwa ujumla.
“Tunashukuru sana tunao ushirikiano mkubwa sanaa wanatutembelea wanatuuliza nini changamoto na kama kuna kitu kikubwa tunatatua na kwenda vizuri kusema kweli tunaenda vizuri sanaa, “alisistiza Abanoor.
“Kwa kweli sera ya viwanda ya Rais Samia imekuwa mkombozi mkubwa sana kwa sisi wawekezaji na tunajivunia kuwa na Rais ambaye ana maono makubwa ya viwanda hali hii itatusaidia kupata mafanikio makubwa katika sekta ya viwanda nchini, “alibainisha Mohammed.
Awali akizungumzia namna wanavyozalisha gesi kiwandani hapo Mkurugenzi huyo alisema wana uwezo wa kuhudumia nchi nzima kulingana na mahitaji yaliyopo huku wakiahidi kuongeza kasi ya uzalishaji.
Alisema kazi yao ni kuzalisha gesi na nitrojen pamoja na liquid zake ambapo hivi sasa wanategemea kuanzisha aina nyingine ambapo mtambo wamekwishaagiza.
Sambamba na hayo alisema wanasambaza gesi katika hospitali zote za wilaya na Mkoa ambapo kazi zao kubwa ni kulinda mahitaji ya viwanda kwani viwanda bila oksijeni haviwezi kufanya kazi na hospitali zao.
“Nawashauri wenye viwanda wengine tuungane kwa pamoja na kujua Tanga yetu nini inataka ili mzunguko uendelee kuwepo hapa hapa kwetu na si sehemu nyingine na kila mmoja kama anabuni kitu aangalie ni kitu gani kimekosekana ndani ya Mkoa ndio alete, “
Aliongeza kuwa kama sisi tulivyofikiria kwamba mkoa wa Tanga unachangamoto ya oksijeni ambayo hapo awali walikuwa wakichukulia Mombasa lakini tumefanikiwa sasa mkoa wetu upo salama kwenye oksijeni na viwanda vyetu hakuna shida yeyote, “alisisitiza Mkurugenzi huyo.
Mkurugenzi huyo alisema mpaka sasa wanakwenda vizuri na wanahidumia mikoa 4 ikiwemo Singida, Morogoro, Tanga, Zanzibar/Pemba na kuwaasa watu wote wenye uhitaji wa gesi hiyo kufika kiwandani hapo au kuagiza kwa njia ya mawasiliano.
Uwezo wa kiwanda ni chupa 9000 sasa hivi Mikoa mitano tunatumia chupa 1500 tu bado wana nafasi ya ziada ya chupa 7,500.
“Nitrojen ni kitu muhimu sana mwanzoni tulianza na Oksijen baada ya hapo tukaanza kuzalisha Nitrojen ambayo tunayo ya kutosha na inawasaidia sana watu wa mifugo katika matumizi yao, “alisistiza.
Alisema Mkoa wa Tanga hauna shida ya liquid Oksijen na Nitrojen kwani ipo ya kutosha ambapo ameishukuru serikali kupitia wizara ya mifugo kwa kuwatembelea kiwandani hapo na kuona umuhimu wa matumizi ya gesi hizo.
“Soko lipo isipokuwa watu wengi hawajajua kama Tanga kuna kiwanda cha kuzalisha Oksijeni ama liquid ya nitrojen niwaambie tu wanatanga na wamikoa mingine wachangamkie uwekezaji huu tulioufanya kwani uhitaji wa gesi ni mkubwa ndani na nje ya nchi, “alisema Mohamed.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato