Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline Iramba
Mwandishi wa Habari,Mathias Canal amechangia madawati 30 yenye thamani ya shilingi 2,100,000, na Vitakasa mikono 20 vyenye thamani ya shilingi 1,400,000.
Ametoa mchango huo Septemba 29, 2023 alipohudhuria mahafali ya 60 ya shule ya msingi Kiomboi Bomani iliyopo katika kata ya Kiomboi, Wilaya ya Iramba mkoani Singida.
Pia Mathias amechangia motisha ya shilingi 500,000 kwa ajili ya walimu katika shule hiyo kutokana na kazi nzuri wanayoifanya ya kuwafundisha wananfunzi shuleni hapo.
Aidha akizungumza katika mahafari hayo aliahidi kuwasomesha watoto wote watakaomaliza darasa la saba na kupata ufaulu wa alama ‘’A’’ kwa kila somo kuanzia wale waliohitimu mwaka huu katika shule hiyo.
Katika hatua nyingine amewapongeza wazazi na walezi wa wanafunzi shuleni hapo kwa kukubali kuchangia kwa hiari baadhi ya mahitaji ya wanafunzi ikiwemo chakula kwa ajili ya wanafunzi ambao wapo katika madarasa ya mitihani.
Alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi kuimarisha ulinzi kwa wanafunzi hao waliofanya mtihani wa darasa la saba kwani bado hawajamaliza elimu ya darasa la saba mpaka pale watakapopata matokeo ya mitihani waliyoifanya.
Pia Mwandishi Mathias Canal ameipongeza serikali kwa kutoa shilingi Mil 40 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa Pamoja na ofisi ya walimu.
Katika mahafali hayo Mwandishi Mathias Canal aliambatana na Diwani wa kata ya Kiomboi Mhe Omary Omary, na Mkurugenzi wa DM PLANET Ndg David Mtengile ambaye amechangia 100,000 kwa ajili ya motisha kwa walimu.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba